Miaka 23 baada ya kuungana tena kwa
Ujeurmani mbili, mabadiliko yanaonekana katika upande wa Ujerumani
mashariki. Miundombinu imekuwa bora ikilinganishwa na magharibi, lakini
tofauti za kiuchumi bado zingalipo.
Kansela Helmut Kohl, ambaye
aliesherekea kuungana tena Ujerumani mbili kwa mara ya kwanza, aliwahi
kuwaahidi wakaazi wa majimbo sita ya Ujerumani mashariki mandhari ya
kupendeza. Lakini katika miaka ya kwanza ya muungano huo, hali ilikuwa
kinyume cha hivyo. Miundombinu chakavu, kufilisika kwa makampuni,
viwango vya juu vya ukosefu wa ajira na kuhama kwa vijana kwa wingi,
kiasi kwamba baadhi ya maeneo yalitishiwa kubaki matupu. Hivi sasa ni
miaka 23 tangu Ujerumani mbili ziungane tena. Je, kuna lililotimia
katika ahadi ya Kohl?
Comments