Katibu mkuu wa zamani wa umoja wa Mataifa Koffi Annan amesema itakuwa 'alama ya aibu' kwa bara Afrika iwapo itajiondoa kutoka mkataba wa Roma uliounda mahakama ya kimataifa inayoshughulikia kesi za uhalifu ICC
Akizungumza mjini Cape Town nchini Afrika kusini,Annan alisema ni viongozi wachache wanaoipinga na kuipiga vita ICC na kuonya dhidi ya kujiondoa katika mahakama hiyo ya kimataifa bila ya kuwa na mfumo mwingine wa sheria mbadala.
Kiongozi huyo wa zamani wa umoja wa Mataifa amesema ikiwa viongozi wa Afrika wataipiga vita ICC,na kujiondoa itakuwa fedheha kubwa kwa kila mmoja wao na nchi zao na kukanusha kuwa ICC ina dhamira ya kuwaandama viongozi wa kiafrika na badala yake kuwashutumu viongozi hao kwa kulinda masilahi yao ya kibinafsi na sio ya waafrika wote.
Comments