Kikosi cha Yanga kinashuka dimbani kucheza na Mtibwa Sugar leo ukiwa ni
mchezo wa kwanza kwa timu zote mbili kwa msimu wa wa 2018/19.
Kuelekea
mechi hiyo itakayopigwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, Mwenyekiti wa
Kamati ya Usajili na Mashindano, Hussein Nyika, ameahidi kuwa Yanga
itauwasha moto mkali.
Nyika
amepata jeuri hiyo baada ya kuwamaliza USM Alger kwenye mchezo wa Kombe
la Shirikisho Afrika uliopigwa Agosti 19 ambapo waliweza kuibuka na
ushindi wa mabao 2-1.
Mwenyekiti
huyo anaamini Yanga itaonesha maajabu zaidi ya yale waliyompatia Alger
kwa kuwa wana malengo ya kurejesha kikombe chao ambacho kilikwenda kwa
wekundu wa Msimbazi, Simba.
Mechi hiyo itachezwa majira ya saa 12 za jioni ambapo pia itakuwa mubashara kupitia king'amuzi cha Azam TV.
Comments