Dr Faustine Ndungulile:Sekta ya Afya nchini ni miongoni mwa sekta muhimu katika serikali ya Awamu ya tano
SERIKALI imesema kuwa sekta ya Afya nchini ni miongoni mwa sekta muhimu
katika serikali ya Awamu ya tano na kuwa ndani ya bajeti hospitali za Wilaya
67 zimejengwa huku hospitali za Rufaa zikiboreshwa.
Naibu Waziri wa Afya Wizara ya Afya, Maendeleo ya jamii,Jinsia,Wazee
na Watoto Dr Faustine Ndungulile amewataka Mfuko wa taifa wa bima ya
afya nchini (NHIF) kuhakikisha 2020 watanzania wote wanapata huduma
ya bima ili kuweza kupata matibabu kwa urahisi na wakati sahihi.
Hayo yamesemwa Dar es Salaam jana na Ndungulile alipokwenda
kukabidhi cheti cha Cheti cha mfumo wa uhakiki ubora wa huduma
cha kiwango cha kimataifa cha ISO ambapo NHIF imeweza kushinda.
Alisema serikali bado inapigania wanachi kununua dawa akiitaja kuwa
ni moja ya changamoto kuna humuhimu wa kutoa huduma za juu iliku
dhidi kushawishi wananchi kujiunga na Mfuko wa taifa wa bima ya
afya nchini (NHIF).
Dr Ndungulile alisema NHIF wanatakiwa kujitanua zaidi ikiwemo kujitangaza
na amewasifu kwa huduma nzuri wanazozitoa kwa wananchi .
“napenda niwapongeze NHIF kwa hatua kubwa mliyofikia ya kutoa huduma kwa
watanzania na nimesikia kutoka kwa mkurugenzi kuwa mpaka sasa mna asilimia
31 ya watanzania wote lakini mikakati yenu ni kufika asilimia 50 kwa mwaka
2020,”alisema Dr Ndungulile.
Naye Mkurugenzi wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) Benard Konga
alisema kuwa wao kama mfuko wa bima kwa sasa wanatoa huduma katika vituo
vingi vya afya na pia wameweza kupata idadi kubwa ya wateja wapya.
Konga alisema kuwa, kwa sasa NHIF wamejitaidi kuboresha huduma ambapo
siku za nyuma mtu kupata kitambulisho ilichukua siku nyingi, kwa sasa
mtu kujiunga inachukua siku 4 hadi 7.
Comments