MKUTANO wa tisa wa vyama vya Wafanyakazi Afrika (OATuu) umemalizika leo Dar es Salaam
na kumpongeza Rais Dkt,John Magufuli kwa kupambana na rushwa na hivyo kuwa mfano
wa kwanza wa guigwa barani Afrika.
Naibu Waziri wa Kazi, Vijana na Ajira Tanzania Mhe.
Antony Mavunde
OATUU imesema tangu Rais Magufuli aingie madarakani Tanzania imekuwa mstari mbele
katika kupambana na rushwa hali inayochangia kupewa sifa na mataifa
mengine hivyo shirikisho
Naibu Waziri wa Kazi, Vijana na Ajira Tanzania Mhe.
Antony Mavunde
Akipokea pokea pongezi hizo Naibu Waziri wa Kazi, Vijana na Ajira Tanzania Mhe.
Antony Mavunde amesema kuwa amepokea kwa shauku kubwa pongezi hizo zilizotolewa
na umoja huo.
"Napokea kwa dhati pongezi hizo na huo ni mfano mzuri kwa wananchi wa Tanzania
kuendelea kuipenda serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Magufuli kwani nchi
za Afrika zimeonesha kutambua juhudi za nchi hii kupambana na rushwa na pia
kuna mapambano mengine katika kutokomeza madawa ya kulevya nchini,"alisema Mavunde.
Mavunde alisema kuwa mkutano huo pia ulijikita kuangalia suala la rushwa mbalimbali
zinavyoathiri maendeleo barani Afrika.
Naye katibu Mukuu wa OATUU Arezki Mezhoud amesema vyama vya Wafanyakazi Afrika
vimekutana nchini kwenye Mkutano wa Tisa huku ikiwa imeelezwa kuwa umechaguliwa
kufanyika Tanzania kwa kuwa shirikisho hilo linaunga mkono juhudi za Rais Dkt.
John Magufuli za kupambana Rushwa na kuwa wangependa kuona Afrika inakuwa pamoja
katikajuhudi za kupinga rushwa.
Wakati huo huo Rais wa chama cha Wafanyakazi nchini (TUCTA) Tumaini Nyamghokya
amesisitiza kuwa mkutano huo pia ulilenga kwenye suala la utawala bora na kuwa
rushwa inachangia kukosekana kwa uwajibikaji na kutotenda haki.
TUCTA imefafanua kuwa rushwa ya kisiasa husababisha viongozi wanaoingia madarakani
kujali masilahi yao hali inayosababisha wananchi kukosa huduma muhimu za kijamii.
Comments