Balozi wa China Wang Ke msaada wa cherehani azungumzia jinsi msaada wa cherehani zitakazo saidia wakina mama kuwainia kiuchumi
Balozi wa China hapa nchini Wang Ke akizungumza na wanahabari jijini Dar es salaam.
Serikali ya China imetoa msaada wa cherehani zitakazo saidia wakina mama kuwainua kiuchumi hasa katika kutekeleza dira ya serikali ya awamu ya tano ya uchumi wa kati wa viwanda kufikia 2020.
Akizungumza jijini Dar es salaam siku chache zilizopita wakati wa hafla ya kukabidhi cherehani hizo kwa wanawake wa mikoa ya Simiyu,Mbeya na Kagera,Balozi wa China hapa nchini Wang Ke amesema kwamba msaada huo unatokana na ushirikiano mzuri wa muda mrefu kati ya Serikali yake na Tanzania.
China imetoa cherehani 73 mkoani Simiyu,cherehani 40 mkoani kagera pamoja na Cherehani 80 mkoani Mbeya kwa ajili ya kuwafanya wanawake wainuke kiuchumi.
Akizungumza wakati akipokea msaada huo ,Mbunge wa Busega mkoani Simiyu Dr.Raphael Chegeni amemshukuru balozi huyo nakusema kuwa uchumi wa kati wa viwanda hauwezi kufanikiwa endapo jamii kuanzia ngazi za chini haitawezeshwa,hivyo msaada huo utasaidia kuanzisha viwanda vya kuzalisha mali mkoani humo.
Kwa upande wake Flora Mathew ambaye ni mwakilishi wa shirika la Women Trust Fund amekabidhiwa cherehani 80 huku akiahidi kuzifikisha kwa walengwa.
Naye katibu mkuu wa shirika la Maendeleo Bukoba( BUDEFO) Tryphon Rutazamba amepokea cherehani 40 na kusema kuwa hatua hiyo ni muendelezo wa historian nzuri ya ushirikiano na China iliyodumu kwa muda mrefu.
Comments