CRDB tawi la Temeke , imeanza
kutoa mafunzo ya maboresho kwa wafanyabiashara wadogo na wakati katika Manispaa
ya Temeke, kwa lengo la kuwajengea uwezo ili waweze kufanya biashara zenye tija
na faida zaidi.
Akifungua mafunzo hayo yaliyotolewa kwa siku tatu mfululizo na kufikia kilele chake
siku ya alhamis wiki hii, Meneja wa CRDB tawi la Temeke Andrew Augastine
aliwataka wafanyabiashara hao kuhudhuria kikamilifu na kuwaalika wengine
kwakuwa hutolewa bure.
“Wafanyabiashara wengi wanashindwa kuendelea na kukuza
biashara zao, kwa sababu mbalimbali,tutawapa mafunzo yatakayo wajenga upya na
kufahamu mazao ya tolewayo na Benki ya CRDB”Alisema.
Lengo la mafunzo hayo nikuwajengea uwezo wafanyabiashara hao ,ili
waweze kufanya biashara zinazo kidhi vigezo vya ubora na zenye kuleta faida
kubwa.
Hata hivyo Augastine ali waahidi wafanyabiashara hao
kuwafungulia akaunti bure na baada ya mafunzo hayo watatunikiwa vyeti vitakavyo
watambulisha kama wafanyabishara waliosoma biashara kwa kiasi fulani.
Naye mhamasishaji wa mafunzo hayo ambaye pia ni Meneja wa wa
kitengo cha biashara ndogo na za kati Claudina William ,aliwataka washiriki
kufuatilia mafunzo hayo kwa umakini ili watakapo maliza mafunzo hayo wawe
wameelewa barabara.
“ Nawaombeni muwe mnafuatilia mafunzo haya kwa umakini wa
hali ya juu ili mtokapo hapa muwe mmetoka na kitu kitakacho badirisha biashara
zenu kutoka hapo zilipo na kupaa zaidi.”Alisema Claudina.
Mafunzo yatakayotolewa na ambayo tayari yalianza kutolewa
jana ni yale ya kufahamu misingi ya uwendeshaji bora wa biashara,jinsi ya
kukuza mtaji,manunuzi ,kutunza kumbukumbu, udhibiti wa mali ,na na jinsi ya
kuandaa mpango wa biashara.
Comments