VYAMA vya Wafanyakazi Afrika vimekutana nchini kwenye Mkutano wa Tisa wa Shirikisho la Vyama hivyo Afrika(OATWU) huku ikiwa imeelezwa kuwa umechaguliwa kufanyika Tanzania kwa kuwa shirikisho hilo linaunga mkono juhudi za Rais Dkt. John Magufuli za kupambana Rushwa.
Hayo yamesemwa jijini Dar es Salaam jana na Katibu wa TUCTA, Yahaya Msigwa kwenye mkutano huo uliokutanisha pia Umoja wa Afrika(AU).
Hayo yamesemwa jijini Dar es Salaam jana na Katibu wa TUCTA, Yahaya Msigwa kwenye mkutano huo uliokutanisha pia Umoja wa Afrika(AU).
Amesema kuwa tangu Rais Magufuli aingie madarakani Tanzania imekuwa mstari mbele katika kupambana na rushwa hali inayochangia kupewa sifa na mataifa mengine hivyo shirikisho likaonelea kuipa heshima.
“Tanzania imepewa heshima ya kufanyika mkutano kwa kuwa inaongoza katika mapambano ya rushwa hasa tangu Serikali ya Awamu ya Tano ilipoingia madarakani,” alisema.
Amebainisha kuwa mkutano huo unajadili maendeleo barani Afrika na kusitisitiza utajikikita katika kuangalia suala la rushwa mbalimbali zinavyoathiri maendeleo barani humo.
Amesisitiza kuwa mkutano huo pia utaegemea kwenye suala la utawala bora endapo usipozingatiwa unavyochangia kukosekana kwa uwajibikaji na kutotenda haki.
Amefafanua kuwa rushwa ya kisiasa husababisha viongozi wanaoingia madarakani kujali masilahi yao hali inayosababisha wananchi kukosa huduma muhimu za kijamii.
Katika hatua nyingine, amesema wanachama wa shirikisho waliokuja kwenye mkutano huo wanatamani kuonana na Rais Magufuli huku akibainisha watatoka na mapendekezo yatakayowasilishwa Serikalini.
Comments