Mkuu wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM), Prof.Tadeo Satta
amemzawadia jumla ya shilingi milioni 2.2 na cheti kwa mwanafunzi
Novath Valerian aliye ongoza katika masomo ya shahada ya kwanza
Chuo ni hapo.
Akikabidhi zawadi hiyo ya fedha mbele ya waandishi wa habari
Dar es Salaam jana Prof. Tadeo amesema kuwa Chuo kimekuwa
na utaratibu wa kuwapatia motisha ya aina hiyo wanafunzi
kwa kuwapa zawadi wanafunzi wanao ongoza.
Amesema wanafunzi wa aina hiyo wamekuwa ni chachu ya kufanikiwa
katika soko la ajira kwani waajili wengi wamekuwa wakiajili
wanafunzi wa aina hiyo mara wanapokwenda katika soko la ajira.
"Maranyingi vyuo vimekuwa vikiwapa zawati wanafunzi na sisi kama
Chuo cha IFM ni moja kati ya chuo kinachotambulika ulimwenguni
hivyo tumekuwa tukitoa zawadi,"alisema Prof Satta.
Prof. Satta alisema kuwa zawadi waliompatia mwanafunzi huyo
ni juudi ya pekee ilikuhamasisha wanafunzi wengine kufanya
vizuri.
Amefafanua kuwa fedha hizo alizopata Novath sh 1,000,000 zimetolewa na
Baraza la Chuo na sh 1,000.000 zimetolewa na yeye Mkuu wa chuo nakua
sh 200,000 zilitolewa na mwalimu Mkufunzi wa Utafiti chuoni hapo.
Akizungumzia upande wa ajira amesema kuwa IFM imekuwa ikitoa
wahitimu wazuri waliobobea katika masuala ya uhasibu katika
mtazamo wa kumudu soko la ushindani wa ajira.
Kwa upande wa Novath amesema kuwa malengo yake makuu
ni kufikia mafanikio zaidi kwa kufika mbali ili
ajekuwa mshauri elekezi katika masuala ya fedha.
"Nape niwe mshauri elekezi katika masuala ya fedha na nasafari
yangu bado inaendelea kutafuta mafanikio,"amesema.
Chuo cha IFM kimeelezwa kuwa tangu 1972 kimekuwa kikitoa
wahitimu wazuri katika ubobezi wa masuala ya uhasibu na
wanao mudu soko la ajira katika ushindani.
Comments