POLISI DAR YAWATAKA WATU WANAOHUJUMU MASHIRIKA YA DAWASCO,TANESCO NA MENGINE KUJISALIMISHA
Kamanda wa Jeshi la Polisi Kanda Maalum,Lazaro Mambosasa akizungumza na wanahabari.
Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam limewataka wananchi kuepuka kuhujumu uchumi wa miundombinu ya makampuni mbalimbali ikiwemo ya Maji,TANESCO pamoja na umeme.
Wito huo umetolewa la jijini Dar es salaam na Kamanda wa Jeshi la Polisi Kanda Maalum,Lazaro Mambosasa wakati akizungumza na wanahabari ambapo amesema kuwa wamebaini kuna baadhi ya wananchi wanahujumu miundombinu ya mashirika hayo kwa kuingina kwenye nyumba zao bila ya idhini ya wahusika.
Kamanda Mambosasa ametoa onyo kwa watu wote wanaojihusisha na kuhujumu miundombinu hiyo kuwa wajisalimishe.
Mkurugenzi wa DAWASCO Mhandisi Cyprian Luhemejaamesema DAWASCO imekuwa ikipoteza maji pasipokukuta yanamwagika barabarani hivyo wanashirikiana na polisi ili kuwabaini watu wanaotumia maji pasipokutoa taarifa kwao.
Leila Muhaji ni Kaimu Meneja Uhusiano TANESCO,amesema hawapendi kuona mtu yeyote anayejihusisha na wizi wowote wa umeme hivyo amelishukuru Jeshi la Polisi kwa kuhakikisha wahujumu wanakamatwa.
Katika hatua nyingine Kamanda Mambosasa amesema Jeshi hilo linaendelea kuwashikilia watu 13 kwa tuhumua unyang’anyi wa kutumia silaha katika maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es salaam.
Comments