NAIBU Meya wa Jiji la Dar es Salaam(CUF) Musa Kafana na Mwanasheria
Mkuu wa Chama cha Wananchi CUF ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu
Hashim Mziray jumamosi wameng'atuka na kutangaza kujiunga na Chama cha
Mapinduzi.
Viongozi tayari wameendeleza wimbi la viongozi wengine waliotangaza nia zao
za kujiunga na CCM wakitokea katika vyama vya upinzani nchini.
Akitangaza rasmi maamzi yake jijini Dar es Salaam juzi bele ya
waandishi wa habari Musa Kafana alisema kuwa
anaipongeza serikali ya chama cha mapinduzi CCM kwa
kuendelea kuwa na ustawi mzuri katika kuendeleza mambo
mbali mbali ya kijamii kwa wananchi wake.
Alisema tangu achanguliwe kuwa Diwani wa Kiwalani
mwaka 2015 ameshirikiana vema na serikali kuleta
maendeleo katika kata hiyo.
"Ukiangalia leo hii kisarawe imekuwa na maendeleo mazuri
na nimekuwa nikishirikiana vema na Mkuu wa Mkuoa wa
Dar es Salaam kuleta maaendeleo yanayoonekana kwa
sasa,"alisema Kafana .
Kafana alisema kuwa moja ya maendeleo aliyoyafanya
katika kuiletea maendeleo Kisarawe ni pamoja na kuwa
kwa sasa Kiwalani kunasoko zuri na vizimba 8 na wanatarajia
ndani ya muda mfupi kuwa na gari la taka.
Alisema pia kwa sasa wanabara bara nzuri ambapo ni muuonekano
wa maendeleo mazuri ya kimsingi katika
maendeleo ya uongozi wake.
"Ilani ya serikali ya CCM imetekeleza mambo ya muhimu
kwani Rais John Magufuli wakati wa kampeni zake 2015,alihaidi
wananchi mambo mazuri katika katika utawala wake na kimsingi
ameyatekeleza,"alisema Kafana .
Kiongozi huyo aliyejitoa CCM alieleza kuwa amejitoa Chama cha
wananchi CUF kutokana na kuwa amekuwa afanyi siasa za utulivu
kutokana na misagano iliyopo ndani ya chama hicho.
"Mimi bado ni kijana nataka niendelee kufanya siasa safi
katika maisha yangu ndio maana nimeomba kuhamia chama cha CCM
kwenye utulivu ambako naona naweza kuendelea kufanya siasa zenye
utulivu,"alisema Kafana .
Naye Mwanasheria Mkuu wa Chama cha Wananchi CUF ambaye ana digrii
ya sheria ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam huku namba yake ya uwakili
ikiwa ni 3932 ambaye pia alikuwa ni Mjumbe wa Kamati Kuu Mziray
ambaye juzi naye alitangaza kung'atuka alisema anafurahishwa na
kujiunga na CCM.
Comments