SERIKALI imesema kulingana na vijana wengi duniani katika nyakati za sasa kuonekana ni tatizo katika kujihusisha na mambo ya uvunjifu wa amani imehimiza kuwapa fursa
NAIBU Katibu Mkuu Wizara Elimu Sayansi na Teknolojia Dk.Ave Maria Semakafu amesema Vijana wakitumiwa vizuri wanaweza kuwa suluhisho la vitendo vya uvunjifu wa amani Barani Afrika.
Dk.Ave Maria aliyasema hayo jana Dk.Ave Maria wakati wa uzinduzi wa utafiti uliofanywa na Idara ya Sayansi ya Siasa ya Chuo Kikuu cha Dar es salaam (UDSM),utafiti ulio hoji “Vijana kujihusisha na matukio ya kihalifu.
“Vijana ni nguvu kazi ya Taifa hivyo wakitumiwa vizuri watakuwa msaada mkubwa katika kukabiliana na matukio ya uhalifu lakini wasipotumika vizuri na kuandaliwa kukua katika maadili ya kumtukuza Mungu watakuwa wakishiriki vitendo hivyo.”Alisema Dk.Ave Maria.
Alisema kuwa asilimia kumekuwepo na wimbi la matukio ya kiuhalifu Barani Afrika hufanywa na Vijana kutokana kuthibitika huko Wataalamu wa tafiti kutoka UDSM wakaona kuna haja ya kufanya tafiti na wamefanya Tafiti hizo na makala nne kutoka Tanzania ndiyo zilikuwa bora kwakuwa zilijikita katika uhalisia wakuhusika kwa vijana.
Katika mkutano huo umezitaja nchi zilizo shiriki kuwa ni Kenya ,Ethiopia ,Uganda, Afrika Kusini, Zimbabwe na Tanzania lakini Jalida (Chapisho) la vyuo Vikuu Afrika limeitangaza Tanzania kuwa ndiyo walioandika makala nzuri kuhusu vijana kujihusisha na masuala ya uvunjifu wa amani barani Afrika.
“Tafiti hizi zilizofanywa na kuthibitishwa na Jalida la Vyuo vikuu Afrika nakuonekana Tanzania tumeandika makala nzuri kwa maana ya uhalisia na siyo kubashiri ni lazima sasa vijana wasaidiwe.”Alisema Dk.Ave Maria.
Kiongozi huyo aliongeza kuwa kwakuwa serikali imetoa vikwazo vyote kwenye elimu watawekeza mkazo zaidi kwenye elimu kwakuwa mtu akielimika atawazua jema na baya kujihusisha katika vitendo viovu ni kuhatarisha maisha yao.
Kwa upande wake Dk.Rasul Minja Mkuu wa Idara ya Sayansi ya Siasa UDSM alisema kuwa vijana siyo bomu linalotaka kulipuka ,bali vijana wakitumika vyema wataweza kuondoa na kukomesha viashiria vya uvunjifu wa amani katika nchi yetu na Duniani kwa ujumla.
“Tumeona tutoe machapisho ya utafiti wetu katika Jalida letu la vyuo vikuu Afrika na tutazitafsiri makala zote kwa Kiswahili na kutoa semina kuanzia ngazi ya serikali ya mitaa hadi Taifa na kuendesha mijadala kwa lengo la kumuelimisha kijana wa kitanzania.
Utafiti huo ulifanyika mwaka jana na kukamilika mwanzoni mwa mwaka huu ,ambapo ulifanyika katika miji mikuu na majiji likiwemo jiji la Mwanza, Arusha na Dar es Salaam na sehemu chache za Mkoa wa Pwani ikiwemo Ikwiriri,Kibiti na Rufiji.
Watafiti hao waliwahoji watu wa kada mbalimbali kama Askari wa Jeshi la Polisi,walioko mahabusu na magereza ,wake wa watuhumiwa, waganga wa jadi , mashehe na wachungaji hususani katika maeneo ya Kibiti , Ikwiriri na Rufiji kutokana na kuripotiwa kwa vitendo vya kiharifu dhidi ya binadamu vilivyokuwa vikiendelea huko mkoani Pwani.
Hitimisho la Utafiti huo ni kujengwa kwa jamii imara itokanayo na vijana ili kuweza kuwa na Taifa imara na lenye watu walio starabika na wasiyo jihusisha na vitendo vya kiharifu.
Comments