SERIKALI nchini imesema kuwa imefanikiwa kujenga mahabara za kisayansi
kwenye shule za sekondari kwa kila halmashauli zote nchini.
Hayo yamesemwa Dar es Salaam juzi na Waziri wa elimu nchini Profesa Joyce
Ndalichako alipokuwa mgeni rasmi kwenye maadhimisho ya wakandarasi wa wanawake
walipo kuwa wameungana na wakandarasi wengine kusherekea miaka 50 tangu
kuanzishwa kwa Bodi ya wahandisi huku benki ya CRDB ikiwa imedhamini maadhimisho
hayo.
Alisema kuwa kuelekea uchumiwa viwanda serikali imekua ikiimiza wasichana
shule ya msingi na sekondari kuyapenda masomo ya hesabati na Sayansi ili
kuja kupata wahandisi wazuri.
"Hadi sasa nchini kunawakandarasi 2026 ambao kati yao asilimia 10 tu no
wanawake hivyo bado tunaitaji jitihada katika kufikia asilimia 50 kwa 50,"
alisema Ndalichako.
Alisema serikali ya tano inawataka watoto wa kike kupenda masomo ya hesabu
na sayansi ili kujakufikia uchumi wa katika maendeleo ya viwanda.
Naye Alice Isibika ambaye ni Mwenyekiti wa kitengo cha wahandisi wanawake(IET)
alisema wamekuwa wakifanya ziara kutembelea baadhi ya shule za msingi na
sekondari kuhimiza juu ya wanafunzi wasichana kupenda masomo ya sayasi.
"Tumekua tukipitamashuleni kusisitiza wanafunzi wa kike kuyapenda masomo ya
sayansi ili tumeanza na shule zilizopo Dar es Salaam na baadaye tunampango wa
kuendelea nchi nzima,"alisema Isibika.
Naye meneja husiano wa mikopo midogo na ya kati wa benki ya CRDB iliyodhamini maadhimisho hayo ya 50 ya
wahandisi nchini Elizabeth John alisema kuwa wamejitokeza kudhamini siku
hiyo kupitia huduma zao za kibenki kama akaunti ya Junior Jumbo ambayo ni
akaunti mahususi kwa wazazi ama walezi.
Elizabeth aliwataka Wazazi kuelewa umuhimu wa akaunti hiyo kwani ni taswira
njema kwa maendeleo ya mtoto pindi atakapo fikia umri wa masomo ya sekondari .
"Akaunti inaweza kufunguliwa kwa shilingi au dola ama euro pamoja na pauni
ambapo kiwango cha chini cha kufungulia ni 20,000 au ,"alisema Elizabeth.
Alisema kuwa gharama ya uendeshaji ni ndogo na pia akaunti hiyo huwajengea
watoto tabia njema ya kupenda kujiwekea akiba ni njia inayo rahisisha zoezi
la kuwekeza fedha kwa ajili ya mahitaji ya mtoto kwa wazazi.
Aidha alisema benki ya CRDB inatoa mikopo mikibwa kwa wafanyakazi yenye
riba na vigezo nafuu kwa waajiri wa serikali,mashirika ya Umma na sekta
binafsi.
Pia alisema mikopo ya wafanyakazi benki hiyo inatumika kwa malengo ya mkopaji
ikiwemo uanzishwaji au uwekezaji katika biashara,kununua nyumba au gari,kulipa
ada au shughulu nyingine yeyote.
Comments