Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto,Ummy Mwalimu
ameipongeza Mamlaka ya Chakula na Dawa(TFDA)
pamoja na Taasisi ya sekta Binafsi nchini (TPSF)kwa kushirikiana kwa
pamoja na wadau wa viwanda vya chakula kukaa na kujadili kwa pamoja namna
nzuri ya kutekeleza kwa vitendo azma ya Serikali ya Awamu ya Tano inayotaka nchi kuwa ya uchumi wa viwanda.
Pongezi hizo amezitoa jijini Dar es Salaam katika Mkutano wa wadau wa chakula kuamasisha uanzishaji na uboreshaji wa viwanda vya chakula na kubainisha kuwa
Tanzania ni nchi yenyefursanyingi za kuwekeza katika eneo la viwanda ikiwa
ni pamoja na viwanda vya chakula.
Amesema hali hiyo inatokana na kuwepo kwa mazingira wezeshi kama vile hali
ya kisiasa ,utashi wa kisiasa na upatikanaji wa malighafi mbali
mbali zinazotumika katika uzalishaji wa chakula.
"Jitiada nyingi zimefanywa na vizara kama kutafuta ada ya ukaguzi wa viwanda
vidogo vidogo vya chakula,ada ya vibali vya kusafirisha chakula nje ada ya
tathmini ya lebo ya bidhaaya chakula,ada ya matangazo ya bidhaa za chakula
pamojana ada ya matangazo ya bidhaa za chakula pamoja na ada ya kudurufu hati
ya usajili wa bidhaa za chakula ,"amesema.
Amebainisha kuwa hakuna hakuna tozo kwa malighafi zinazoingizwa
nchini na wenye viwanda vya kusindika.
Amefafanua hadi sasa kuna viwanda nane ambapo kufikia Desemba mwaka huu
watakuwa wamepunguza idadi kubwa ya fedha za nchi kwenda kununua dawa.
Aidha amesema TFDA imeanza njia nyingine ya kutoa ushauri na kuwa
wasajili wa majengo kwa ambapo kwa sasa hauzidi zaidi ya siku 10.
Kwa upande wake, Waziri wa Viwanda,Biashara na Uwekezaji Charles Mwijage amedodosa kuwa viwanda vinavyojengwa ni kwaajili ya kuzalisha ajira na
viwanda hivyo vikiwa vingi vinaongeza na vitasaidia kodi kushuka
kutokana na kuwa wananchi wengi watakuwa na ajira.
Ameongeza kuwa taasisi za serikali zinapaswa kushirikiana na amewata
wenye mitaji midogo ya kuzalisha bidhaa kama tomato sauce
waende wakapewe vyumba SODO na pia amewashauri wananchi
katika kuelekea Tanzania ya viwanda wajenge viwanda na si
nyumba za kupangisha ili kwendana na wakati huu ambapo
kwa sasa nyumba za kupangisha hazina soko .
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa mamlaka hiyo, Agnes Kijo amesema TFDA itaendelea kushirikiana bega kwa na wadau hao ili kuhakikisha azma ya uchumi wa viwanda inafikiwa huku akisisitiza watahakikisha bidhaa za chakula zinakuwa ubora na usalama kwa walaji.
Comments