Mwanachama na aliyekuwa Mwenyekiti wa klabu ya Yanga, Yusuph Manji,
ameshindwa kuungana na wachezaji wa klabu hiyo kwa ajili ya kujumuika
nao kula mlo wa usiku baada ya kufikia kwenye hoteli ya Protea iliyopo
maeneo ya Posta, jijini Dar es Salaam.
Yanga iliwasili hotelini hapo ikitokea Morogoro ambako ilikwenda kuweka
kambi ya wiki mbili kwa ajili ya kujiandaa na mchezo wa Kombe la
Shirikisho Afrika dhidi ya USM Alger kutoka Algeria.
Awali uongozi ulieleza angeweza kufika hotelini hapo kwa ajili ya
kujumuika nao lakini imekuwa sivyo na haijajulikana sababu za kushindwa
kuwasili kwa Manji ni zipi.
Mbali na kushindwa kuwasili hotelini hapo, Manji anategemewa kuhudhuria
mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika ambapo Yanga itacheza dhidi ya USM
Alger majira ya saa 1 jioni leo kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Yanga itashuka dimbani kukipi
Comments