Na Hussein Ndubikile,Pwani
Mwenyekiti wa Baraza la Ardhi na Nyumba la Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga Mkoa wa Pwani, Rehema Mwakibuja amewaondoa wadaiwa wawili akiwemo Omari Issa na Bakari Saguti katika kesi ya msingi ya mgogoro wa ardhi kati ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali(AG), Adelardus Kilangi ambaye ni mdai dhidi ya wadaiwa zaidi ya 70 ambao ni wananchi wa Kijiji cha Vicheji kilichopo wilayani humo licha ya wadaiwa hao kudai hawawezi kutoa maelezo sababu kuwa Wakili wao hayupo.
Hatua hiyo imekuja baada ya wadaiwa hao kutakaa kutoa maelezo kwa kuwa wakaili wao alipata ajali na taarifa walishatoa huku kila mmoja akisisitiza tayari wameshafanya mazungumzo ya awall na wakili mpya hivyo tararibu zitakapokamilika wataaendelea na kesi.
Mwenyekiti wa baraza hilo alituipilia mbali ombi hilo kwa kueleza kuwa kesi imeshaletwa mezani hivyo lazima iendelele kusikilizwa na kwamba waliokataa kuzungumza amewafuta majina yao.
Kwa upande wa mdaiwa, Juma mauge alipotakiwa kutoa maelezo alidai hawezi kuongea kwa ufasaha kwa ametoka kwenye msiba wa mama yake mzazi, hivyo mwenyekiti alimkubalia na kumtaka aende akajiandae atapokuja kesi iendelee kusikilizwa.
Katika hatua nyingine mwenyekiti huyo aliwaambia wadaiwa waliofika katika baraza hilo hakuna sheria inayoelezea wadaiwa kutoa maelezo kwa mtiririko wa watu waliowapanga hivyo baraza hilo lina uwezo wa kumchagua yeyote kati yao na si vinginevyo.
Mgogoro katika kesi namba 55 ya mwaka 2016 unawahusisha wadaiwa Said Kaisi 46, Bakari Saguti 60, Omary Issa 42, Juma Omary 40, Salima Bilali (53), Regia Issaya(55) ,Sada Abdallah(72) na ambao kwa pamoja wanadaiwa kuingia kwenye shamba la Kilangi bila kibali.
Washitakiwa hao kwa pamoja inadaiwa kuwa Mei 9 2016 katika Kijiji cha Vicheji waliharibu Miti 13 ya Minazi na nyumba mbili vyenye thamani ya Sh. Mil 22.2 mali ya AG Kilangi.
Kesi hiyo imeahirishwa hadi Agosti 15 mwaka huu itakapokuja kwa ajili ya kuendelea kusikilizwa.
Comments