Mamlaka ya
Usafiri wa Nchi Kavu na Majini nchini (Sumatra) imefanya mazungumzo na Chama
cha Reli cha Nchi Kusini mwa Afrika (Sara) ili kuhakikisha nchi wanachama
zinakuwa na wadhibiti wa reli wenye
viwango vinavyofanana pamoja na kuongeza
usalama.
Hayo
yamesemwa leo jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Mtendaji wa Sumatra Giliard
Ngewe wakati akizungumza na wanahabari.
Amesema
mazungumzo hayo yamefanyika kutokana na
nchi wanachama kukosa wadhibiti wa reli wasio na viwango vinavyofanana huku
akisisitiza kuna wadhibiti wa reli wawili tu katika nchi zinaounda SADC.
“Lengo la
Majadiliano ni kuhamasisha nchi nyingine za kusini mwa Afrika ziwe na wadhibiti
wenye viwango sawa maana hadi sasa tuna wadhibiti wawili tu,” amesema,”.
Amebainisha
kuwa katika mazungumzo ya majadiliano hayo watatoka na maazimio ya jinsi ya
kuungana na kutumia viwango vya udhibiti vinavyofanana.
Kwa upande
wake,Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Dk, Leonard
Chamuriho amesema pasipokuwepo na wenye viwango vinavyofanana viwango vya
udhibiti wa reli hutofautina na kuongeza nchi za SADC zinatakiwa kutekeleza
ajenda ya Umoja wa Afrika ( AU)
inayozitaka ziwe na reli za kisasa zinazofarisha mizigo mizito.
Amesisitiza
kuwa nchi zote za SADC zinatakiwa ziwe na viwango sawa vya udhibiti wa reli na
kubainisha kwamba usafirishaji wa mizigo unaotumia reli hauna gharama.
Naye Rais wa
Sara, Babe Botana amesema lengo liliowakutanisha ni kuhakikisha viwango vya
wadhibiti wa nchi wananchama wa SADC vinafanana na usafiri wa reli unakuwa wa
kisasa.
Comments