WAFANYABIASHARA wadogo, wakati na wakubwa wa benki ya CRDB, Tawi la Temeke Jijini Dar es Salaam wametakiwa kuchangamkia fursa za mikopo zitolewazo katika Tawi hilo.
Meneja wa CRDB Temeke, Andrew Augustine aliyasema hayo mwishoni mwa wiki wakati, alipokuwa akifunga mafunzo ya maboresho kwa wafanyabiashara wa Manispaa ya Temeke yaliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Chuo cha Utalii Tandika jijini humo.
Alisema kuwa amewataka wafanyabiashara hao kutumia fursa hiyo yakujipatia mkopo kupitia tawi la CRDB Temeke kwa riba nafuu ya 19% na kuwahakikishia kuwa hakuna ukiritimba katika utoaji wa mikopo katika Benki hiyo inayoongoza kwakutoa huduma za kibenki nchini.
Alisema kuwa amewataka wafanyabiashara hao kutumia fursa hiyo yakujipatia mkopo kupitia tawi la CRDB Temeke kwa riba nafuu ya 19% na kuwahakikishia kuwa hakuna ukiritimba katika utoaji wa mikopo katika Benki hiyo inayoongoza kwakutoa huduma za kibenki nchini.
“Kwa habari njema ya wafanyabiashara wadogo, wakubwa na wakati Mkurugenzi Mkuu wa CRDB Dk. Charles Kimei, ameitdhinisha Sh Bilioni 2, kwa ajili ya kuwakopesha wafanyabiashara wa CRDB Temeke lakini mwitikio ni mdogo,"Alisema Augustine
Wakati huo huo Augustine aliwatoa hofu wafanyabiashara hao kuhusu uchumi wanchi nakusema kuwa uchumi wa Tanzania upo imara na madhubuti na kuongeza kuwa shilingi imerudi kwenye mzunguko wake ikilinganisha na miaka 2 iliyopita.
“Mdororo wa mzunguko wa kifedha kwa sasa umeimarika ukilinganisha na miaka miwili iliyopita , hii ni kutokana na Serikali kulipa baadhi ya madeni nakufanya mzunguko wa shilingi kurejea mataani.Njoo CRDB tutakupa ushauri jinsi ya kusonga mbele,"Alisema.
Naye Meneja wa Bishara na huduma za kibenki CRDB Temeke, Burtony Mbogella, aliwaasa washiriki kutokuwa wanyimi wa taarifa na kuwataka kufikisha ujumbe kwa wenzao ambao hawakushiriki mafunzo hayo kutokana na sababu mbalimbali.
Hata hivyo Mbogella aliwataka washiriki hao kuunda kundi moja ambalo litawasaidia kupewa kipaumbele wakati watakapo hitaji mkopo na huduma nyingine za kibeki.
“Undeni jina la kundi ili mnapokuja CRDB Temeke mnajitambulisha kwa jina la kundi lenu inakuwa rahisi kuwadumia kwakuwa tulishawapa mafunzo tunawaamini.” Alisema
Naye Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Temeke Rukia Kamal akisoma risala kwa niaba ya washiriki wa mafunzo hayo ambayo naye alishiriki kama mfanyabiashara aliipongeza CRDB kwakuendesha mafunzo hayo bure.
Rukia aliwaomba CRDB Temeke kuendelea kutoa mafunzo hayo kwa wananchi wa Temeke kwakuwa Temeke ni kubwa ikilinganisha na idadi ya watu waliofikiwa kupitia mafunzo ya biashara,mikopo na mbinu za kukuza mtaji.
“CRDB Temeke muendelee kuwapa mikopo wafanyabiashara wetu kwakuwa maisha ya wananchi wa Temeke ni duni hivyo ningependa kuona maisha ya wananchi hao yanaimarika kiuchumi .”Alisema
Rukia amelielezea gazeti la Majira kuwa baada ya mafunzo hayo kuwa yeye anasimamia ilani ya CCM ambayo imeelekeza bayana kuwainua wanachi kiuchumi nakuongeza kuwa atawashawishi wanachi wengi hususani wakina mama kuchangamkia fursa pasipo kujali itikadi za vyama vyao.
Kwa upande wake Muwezeshaji wa mafunzo hayo Claudiana Wiliam ambaye pia ni Meneja wa kitengo cha Ujasiriamali na wafanyabiashara wadogo ,wakati akiwapongeza washiriki kwakushiriki kwa wingi tofauti na walivyo tarajia.
“Kutoka moyoni nimefarijika kuona wananchi wa Temeke mkishiriki kwa wingi ni waombe wakati mwingine mshiriki kwa wingi zaidi ya hivi mlivyoshiriki,'alisema Claudiana .
Washiriki katika mafunzo hayo walipatiwa vyeti kama sehehemu ya kuthamini ushiriki wao katika mafunzo hayo lakini pia vyeti hivyo vilithibitisha ushiriki wao kikamilifu wakati huku CRDB Temeke ikiwafungulia akaunti za biashara wafanyabiashara hao ambao hawakuwa na akaunti za CRDB bila malipo.
Comments