Mwenyekiti wa Baraza la vyama vya siasa Tanzania Magalle John Shibuda
Imeelezwa kuwa mfumo wa vyama vingi vya siasa nchini,utaendelea kuwepo ili kujenga ustawi wa maendeleo ya jamii na uchumi wa taifa.
Mwenyekiti wa Baraza la vyama vya siasa Tanzania Magalle John Shibuda ameeleza hayo leo jijini Dar es salaam wakati akizungumza kwenye mjadala na vingozi na wadau mbalimbali wa siasa nchini kuhusu mabadiliko ya kikatiba na kisheria kuhusu uchaguzi kabla ya uchaguzi mkuu mwaka 2020.
Shibuda amesema kuwepo kwa mfumo wa vyama vingi hujenga kuundika kwa mifumo imara ya uwajibikaji kwa serikali.
“Duniani kote daima uhai mfumo wa vyama vingi utadumu kwa sababu hakuna chama kamilifu dhidi ya kasoro za udhaifu wa kuundwa na desturi za tabia binafsi za mapungufu ya viongozi wa vyama hivyo mfumo wa vyama vingi utaendelea kuwepo ili kujenga ustawi wa maendeleo ya jamii na uchumi wa taifa”amesema Shibuda
Mussa Kombo Mussa ni Makamu Mwenyekiti wa Jukwaa la Katiba (JUKATA) amesema lengo lao ni kushirikiana na vyama vya siasa ili kuishauri serikali kufanyia kazi mapendekezo yao kuhusiana na katiba.
Amesema NEC inapaswa kusimamia chaguzi zote ukiwemo uchaguzi wa serikali za mitaa kwa kuwa uchaguzi huo ni chaguzi kama zilivyo chaguzi za udiwani,Ubunge na Urais
Na baadhi ya viongozi wa vyama vya siasa Katibu Mkuu wa Chama cha Tanzania Labour Part TLP Nansi Mrikaria pamoja na Katibu Mkuu wa SAU,Kisena Fred Kisena ambao wamejitokeza kwenye mjadala huo wamesema umewajengea kujadili mambo yatakayosaidia kujenga demokrasia makini.
Hata hivyo kwa mujibu wa JUKATA imeeleza kuwa kufuatia wimbi la wabunge na madiwani kuhama vyama kwa sababu mbalimbali na malalamiko ya watanzania kuhusu gharama zinazotumika kwenye chaguzi ndogo, wametafakari na kuona ipo haja ya kuruhusu mfumo wa wanasiasa kuhama vyama pasipokupoteza nafasi zao za kuchaguliwa.
Comments