Makampuni matano kutoka Korea Kusini na China wameonesha nia ya kuwekeza kwa kujenga viwanda vya kutengeneza madawa na vifaa tiba.
Makampuni hayo yameonesha nia ya kuwekeza baada ya Mkurugenzi wa Mtendaji wa kituo cha Uwekezaji (TIC)Geoffrey Mwambe kwenda nchini Korea Kusini pamoja na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu kushiriki kongamano la biashara na uwekezaji liliofanyika China Agost I6 mwaka huu kwa ajili ya kuhamasisha wawekezaji.
TIC katika kuwajenga wajasiriamali kimetaja kuwa uwekezaji ndio njia sahihi
ya kufikia uchumi wa viwanda kwa kuzingatia hilo kimetaja kuwa ni wazi kwamba
wanajukumu la kujenga sekta binafsi ambayo ni nyenzo kuu katika uwekezaji.
kizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana Mwambe alisema kuwa
kupitia ziara ya kikazi aliyofanya mwezi huu nchini Korea kusini wamefanikiwa kuhamasisha wawekezaji na kuonesha nia ya kuwekeza.
Alisema kuwa akiwa korea ameshiriki kongamano la Biashara na Uwekezaji lililofanyika Agosti I3 mwaka huu ambapo wafanyabiashara walijadili fursa za uwekezaji katika sekta ya madawa na vifaa tiba.
Ameeleza kuwa katioa ziara hiyo aliongozana na wawakikishi wa taasisi za serikali, Makapuni binafsi, Viongozi wa Chama Cha Watengenezaji na Wauzaji wa Madawa (TAPI) kwa ajili kupanua wigo wa Uwekezaji hapa nchini.
"Makongamano haya yaliambatana na ziara za kutembelea viwanda vinavyomilikiwa na baadhi ya makampuni ambayo yameonesha nia ya kuja kuwekeza Tanzania" alisema Mwambe.
Hata hivyo alisema kuwa miongoni mwa mafanikio ambayo yamepatikana akiwa korea ni pamoja kusainiwa hati za maafikiano (MOU) tatu kati ya TAPI na wafanyakazi wa makampuni ya China ili kuwezesha mafanikio na makampuni ya Tanzania kuwekeza kwa ubia katika sekta ya Afya.
"Lengo la kushiriki magongamano hayo ni kuleta mapinduzi ya uchumi hapa Tanzania" amesema Mwambe.
Katika hatua nyengine Mwambe alifafanua kuwa Kituo cha Uwekezaji kinaendelea kufanya kuboresha huduma za mahali pamoja (One stop facilitation Centre) ili kuwahudumia wawekezaji kwa ufanisi mkubwa.
Amesema kuwa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) pamoja na taasisi nyingine za serikali tayari WAPO katika Ofisi TIC ili kutoa huduma kwa haraka hasa kwa wawekezaji wanaotoka nje ya nchi.
Katika kutengeneza Mazingira rafiki kwa wawekezaji taasisi zote ambazo zinafanya kazi kwa ukaribu na TIC ili kuhakikisha Tanzania ya viwanda inafanikwa na kupiga hatua katika masula mbalimbali yendeleo.
Comments