Jeshi nchini uganda limeomba msamaha kutokana na kitendo cha askari wake kuonekana kwenye video akimpiga mwandishi
Jeshi nchini uganda limeomba msamaha kutokana na kitendo cha askari wake
kuonekana kwenye video akimpiga mwandishi wa habari ambaye alikuwa
akitimiza wajibu wake kwenye maandamano ya kushutumu kukamatwa kwa
mbunge Bobi Wine Agosti 20 mwaka huu.
Mkuu wa Vikosi vya Ulinzi (CDF), Jenerali David Muhoozi, ameagiza askari
waliohusika kuwapiga wanahabari waliokuwa wakitimiza majukumu yao
kukamatwa.
Mbali na hatua hiyo ya jeshi hilo jumuiya ya kimataifa zimeshaanza
kuwashutumu askari wa Jeshi la Ulinzi (UPDF) kwa ukatili na manyanyaso
ya waandishi wa habari ambao walikuwa wakiandika habari za kampeni
katika Jimbo la Manispaa ya Arua hivi karibuni.
Imeelezwa kuwa kisa cha kukamatwa kwa wanasiasa na kuibuka vurugu katika maeneo mengi ya jiji la Kampala Jumatatu.
Msemaji wa UPDF Brigeduia Richard Karemire katika taarifa yake aliyoitoa
kwa vyombo vya habari amesema uongozi wa jeshi unalaani ukatili
uliofanywa na askari wake.
“Uongozi wa UPDF umefahamishwa kuhusu utendaji kazi usiozingatia weledi
wa askari wake waliowasumbua wanahabari waliosambazwa kwa ajili ya
kufuatilia operesheni ya pamoja katika jiji Jumatatu ya Agosti 20, 018,”
ilisema sehemu ya taarifa Brigedia Karemire iliyosambazwa Jumanne.
“UPDF linapenda kueleza kwamba halijafurahishwa na tabia hiyo
iliyofanywa na askari hao binafsi, na kwa sababu hiyo Mkuu wa Vikosi vya
Ulinzi (CDF) ameamuru wakamatwe na waadhibiwe.
Waandishi waliokumbana na mkono katili wa askari wa vikosi vya usalama
ni wanahabari wanne wa televisheni ya NTV; Juma Kiirya, Herbert Zziwa,
Ronald Muwanga, Ronald Galiwango, na wenzao Julius Bakabaage (NBS),
James Akena (Reuters), Samuel Kyambadde (Metro FM) na Richard (Ghetto
TV).
Comments