Na Mwandishi Wetu Aliyekuwa mmiliki wa IPTL Harbinder Singh Sethi ameieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa ana miezi 6 hajaonana na mke wake. Sethi ambaye yupo katika gereza la Ukonga ameyaeleza hayo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Huruma Shaidi baada ya Wakili wa serikali Mwanaamina Kombakono kueleza kuwa kesi ilipangwa kwa ajili ya kutajwa. Baada ya Wakili Kombakono kueleza hayo, Wakili wa Sethi, Dorah Mallaba aliieleza mahakama kuwa bado hawajapata kibali kwa ajili ya mshtakiwa Sethi kuonana na mkewe. Hata hivyo Wakili Mallaba aliiomba mahakama iruhusu hata kwa dakika 5 Sethi aonane na mkewe. “Naomba mahakama itumie busara kwa kuwa mke wake yupo hapa mahakamani, aweze kuonana naye hata kwa dakika 5,”ameomba. Wakili Kombakono baada ya kusikiliza hoja ya wakili Mallaba, alieleza kuwa kuna taratibu za kumuona mah...