Musa Hassan Mgosi, Ayoub Hassan Isiko
Mchezaji
Musa Hassan Mgosi ameombewa usajili Ruvu JKT kutoka DC Motema Pembe ya
Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC), na Ayoub Hassan Isiko ameombewa
usajili Mtibwa Sugar kutoka Bull FC ya Uganda. Wachezaji hao
hawaruhusiwi kuchezea timu hizo mpaka Hati zao za Uhamisho wa Kimataifa
(ITC) zitakapokuwa zimepatikana.
Toto dhidi ya Kagera Sugar kumsaini Enyinna Darlinton Ariwodo
Toto
Africans ilipinga usajili wa Enyinna Darlinton kwa timu ya Kagera Sugar
kwa vile bado ina mkataba wa mchezaji huyo ambao unamalizika mwakani.
Kwa upande wake Kagera Sugar ilisema imemsaini mchezaji huyo kwa vile
Toto Africans imeshindwa kumlipa mshahara ambapo kuna makubaliano rasmi
kati ya Ariwodo kuwa klabu hiyo ikishindwa kumlipa mshahara anaruhusiwa
kuondoka. Uamuzi wa Kamati ni kuwa Ariwodo ni mchezaji halali wa Kagera
Sugar kwa vile Toto Africans ilishindwa kutimiza masharti ya mkataba.
Ramadhan Chombo ‘Redondo’
Redondo
ameidhinishwa kuchezea Simba kwa kuzingatia mchezo wa haki na uungwana
(Fair Play) baada ya klabu hiyo na ile ya Azam kufikia makubaliano
kuhusu mchezaji huyo.
Mchezaji David Luhende kusajiliwa Yanga
Yanga
ilikiri kutolipa ada ya uhamisho ya sh. milioni 5 kama walivyokubaliana
na Kagera Sugar. Awali waliipa Kagera Sugar hundi iliyogonga mwamba
benki (bounced cheque). Shauri hilo lilimalizwa kwa Yanga imetakiwa
kulipa fedha hizo ndani ya siku 21 kuanzia Septemba 10 mwaka huu.
Super Falcon dhidi ya Edward Christopher kusaini Simba
Simba
imepewa siku 21 kuanzia Septemba 10 mwaka huu iwe imeilipa Super Falcon
fedha za matunzo (compensation) kwa vile ndiyo iliyomlea mchezaji
Edward Christopher aliyesajiliwa katika klabu hiyo.
Toto Africans dhidi ya Mohamed Soud kusajiliwa Coastal Union
Toto
Africans iliweka pingamizi kwa maelezo kuwa bado ina mkataba na
mchezaji huyo. Hivyo kwa msingi wa Fair Play, mchezaji huyo
ameidhinishwa Coastal Union baada ya makubaliono kati ya klabu.
Rollingstone dhidi ya Kigi Makassy kusajiliwa Simba
Simba
imetakiwa kuilipa Rollingstone gharama za matunzo ilizoingia wakati
ikiwa na mchezaji huyo kwa kuzingatia kanuni za Shirikisho la Kimataifa
la Mpira wa Miguu (FIFA).
Super Falcon dhidi ya Sultan Juma Shija kusajiliwa Coastal Union
Uamuzi
wa Kamati ni kuwa Shija atachezea Coastal Union, na kwa vile yuko chini
ya umri wa miaka 23, Coastal Union itailipa Super Falcon fidia ya fedha
ilizotumia kumhudumia mchezaji huyo.
African Lyon dhidi ya Razak Khalfan kusaini Coastal
Lyon
imesema bado ina mkataba na mchezaji huyo. Kamati imebaini kuwa mkataba
wa mchezaji huyo na Lyon umemalizika, hivyo ni mchezaji halali wa
Coastal Union.
Flamingo dhidi ya Kelvin Friday kusajiliwa Azam
Friday
ruksa kucheza Azam, lakini klabu hiyo imepewa siku 21 kuanzia Septemba
10 mwaka huu kuilipa Flamingo gharama za kuvunja mkataba.
Super Falcon dhidi ya Robert Joseph Mkhotya kusaini African Lyon
Lyon
imeagizwa kuilipa Super Falcon sh. milioni moja ikiwa ni fidia ya
kuvunja mkataba wa mchezaji huyo ambaye imemsajili. Fedha hizo zitalipwa
kwa awamu nne kutokana na makato ya mlango yatakayofanywa na TFF.
Falcon itapokea malipo hayo kupitia TFF.
Oljoro JKT dhidi ya Othman Hassan kusajiliwa Coastal
Kwa
mujibu wa rekodi za TFF, mkataba wa mchezaji huyo na Oljoro JKT
unamalizika mwakani. Hivyo, Othman Hassan ni mchezaji halali wa Oljoro
JKT kwa vile bado ana mkataba na klabu hiyo.
Yanga dhidi ya Simba kuacha wachezaji wanne
Kamati
imetupa pingamizi hizo kwa vile hakuna malalamiko yoyote kutoka kwa
wachezaji juu ya kuvunjiwa mikataba yao. Wachezaji hao walioachwa na
Simba ni Dan Mrwanda, Haruna Shamte, Kanu Mbiavanga na Lino Masombo.
Ikiwa wachezaji hao watakuwa na malalamiko kuhusu kuvunjiwa mikataba
suala hilo litafikishwa katika Kamati kwa ajili ya kusikilizwa na
kutolewa uamuzi.
Mbuyu Twite
Kwa
mujibu wa Ibara ya 18(3) ya Kanuni za Hadhi na Uhamisho wa Wachezaji wa
Kimataifa za FIFA, Yanga ilifuata taratibu zote katika kumsajili Mbuyu
Twite, hivyo ni mchezaji wake halali. Hata hivyo, kwa vile Yanga imekiri
kuwa mchezaji huyo alichukua dola 32,000 za Simba na kukiri
kuzirejesha, kwa msingi wa kanuni ya Fair Play, Kamati imeipa Yanga siku
21 iwe imelipa fedha hizo Simba.
Kelvin Yondani
Kwa
mujibu wa Ibara ya 44(3) ya Kanuni za Uhamisho wa Wachezaji za TFF,
Yanga ilifuata taratibu zote katika kumsajili Kelvin Yondani, hivyo ni
mchezaji wake halali.
Kwa vile Simba imesema mchezaji
huyo vilevile alisaini mkataba na klabu yao, imetakiwa kupitia mamlaka
nyingine kuthibitisha hilo, na baada ya uthibitisho iwasilishe
malalamiko yake kwenye Kamati ya Sheria, Maadili na Hadhi za Wachezaji,
au mamlaka zozote za kisheria kwa mujibu wa madai/lalamiko husika.Inatoka kwa mdau.
Comments