=WAZIRI Mkuu, Mizengo Pinda, amesema
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kiko jirani na Chama cha
Mapinduzi (CCM). Pinda alitoa kauli hiyo juzi wilayani hapa kabla ya
kuanza ziara yake katika Vijiji vya Bugulula na Senga wilayani Geita kwa
ajili ya kuzindua miradi ya maendeleo.

Katika
kijiji cha Bugulula, Waziri Mkuu alizindua mradi wa ufugaji wa kisasa
wa nyuki na Senga alifungua jengo la kliniki ya baba, mama na watoto.
Wakati Waziri Mkuu akitoa kauli hiyo, alikuwa akimtambulisha Mbunge wa Bukombe, Profesa Kulikoyela Kahigi (CHADEMA).
Baada ya kauli hiyo, baadhi ya viongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na serikali walionekana kucheka.
āMkuu wa Mkoa, ngoja, ngoja
kwanza, Profesa Kahigi hebu simama, unajua wengi hawakujui, ndugu zangu,
huyu hapa (Profesa Kahigi) ni Mbunge mwenzangu ingawa yeyƩ yuko Jimbo
la Bukombe, kupitia kile chama kilicho jirani yetu.
āHamuwezi kuamini, pamoja na
kwamba ni Mbunge kupitia hiki chama kilicho jirani yetu, ninachotaka
kusema ni kwamba huyu ni rafiki yangu mkubwa, tena naweza kusema hakuna
rafiki yangu mkubwa kama ilivyo kwa Profesa Kahigi,āalisema Waziri Mkuu
Pinda na kusababisha viongozi wote waliokuwa eneo hilo kuvunjika mbavu
kwa kicheko.
Comments