Mkuu wa harakati za kudumisha amani wa Umoja wa mataifa Herve
Ladsous ameliambia baraza la usalama la Umoja huo kwamba waasi wameidhinisha
kile anachokiita kuwa ni utawala wa kimabavu Mashariki mwa Jamhuri ya
Kidemokrasi ya Congo.
Bwana Ladsous amesema waasi wa M23 wanadhibiti idadi kubwa ya maeneo ya Mashariki mwa Congo na wanawatoza kodi wananchi .
Umoja wa Mataifa unaishutumu Rwanda kuwaunga mkono waasi wa M23. Wakati huo huo Maafisa wa Congo wanataka Rwanda iwekewe vikwazo biashara ya madini .
Zaidi ya watu 200,000 wameachwa bila makao kufuatia mapigano Mashariki mwa nchi.
Comments