Skip to main content

Chadema Wamlima Barua JK


WAMTAKA ACHUKUE HATUA DHIDI YA MAUAJI YA RAIA KINYUME CHAKE SERIKALI INAHUSIKA
 CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimemwandikia barua Rais Jakaya Kikwete kikimtaka achukue hatua dhidi ya matukio kadhaa ya mauaji ya raia yaliyotokea kwa nyakati tofauti katika mikutano yake ya hadhara kwenye Mikoa ya Singida, Tabora, Arusha, Morogoro, Iringa. Hatua kilichopendeza ni pamoja na kuwawajibisha viongozi wenye dhamana; Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi, Mkuu wa Polisi, IGP Said Mwema; Mkuu wa Operesheni Maalumu Polisi, Paul Chagonja, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Faustine Shilogile na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa, Michael Kamuhanda. Barua hiyo ya Septemba 10, mwaka huu iliyoandikwa na Mwenyekiti wake, Freeman Mbowe baada ya kikao cha Kamati Kuu ya chama hicho, imemtaka Rais Kikwete kuwafukuza kazi watendaji hao katika Serikali yake kwa kuwa wameshindwa kazi. Kimesema kwamba mauaji mengi miongoni mwa hayo, yametokea bila hatua stahiki za kisheria kuchukuliwa na kusema kwamba ukimya huo unaweza kutoa picha potofu kwa umma kwamba Serikali yake inaunga mkono au imewatuma polisi au watu wengine waliosababisha mauaji hayo.

 Matukio ya vifo ambayo chama hicho kimetaka yachunguzwe ni pamoja na lile la Januari Mosi, mwaka jana mkoani Arusha, Igunga (Novemba, mwaka jana) na Arumeru Mashariki (Aprili, mwaka huu). Mengine ni lile la Iramba lililotokea Julai 14, mwaka huu, Morogoro (Agosti 27, mwaka huu) na Iringa Septemba 2, mwaka huu ambalo hata hivyo, shauri lake limeshafikishwa mahakamani. Kimedai kwamba katika Uchaguzi mdogo wa Arumeru Mashariki, Kiongozi wa Kata wa chama hicho, Msafiri Mbwambo alichinjwa huku chanzo cha kifo hicho kikielezwa kuwa ni masuala ya kisiasa.
 Pia kilielezea mauaji yaliyotokea katika Kijiji cha Ndago, Wilaya ya Iramba, Singida na kudai kwamba kikundi cha watu kilivamia mkutano wa Chadema kwa mawe na kwamba licha ya polisi kuwapo eneo hilo, hawakuchukua hatua zozote. Chama hicho pia kimekumbusha mauaji ya mfuasi wake mkoani Morogoro, Ally Zona kikisema kifo hicho pia kina utata kwani taarifa ya polisi imesema alikufa kwa kugongwa na kitu kizito wakati chama hicho kikidhani kwamba alipigwa risasi.
 Kimesema pamoja na matukio yote hayo, viongozi wote hao hawakuchukuliwa hatua zozote za kuwajibika kwa matukio hayo. Pia Chadema kimeonya kuwa hali hiyo ikiachwa inaweza kujenga dhana potofu kwa wananchi kuwa Jeshi la Polisi liko mikononi mwa CCM na kazi yake ni kulinda masilahi ya chama hicho kwa gharama yoyote ile jambo ambalo Mbowe alisema ikiwa Rais Kikwete atachukua hatua za kinidhamu dhidi ya viongozi hao, atakuwa ameudhihirishia umma kwamba Serikali yake haifumbii macho mauaji yanayofanywa na vyombo vya usalama nchini. Kimemtaka Rais Kikwete kuunda tume ya kijaji au kimahakama kuchunguza vifo vilivyotokea katika mikusanyiko, mikutano, maandamano au mazingira ya kisiasa yanayokihusisha Chadema.
Ikulu yajibu Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue alipoulizwa juu ya barua hiyo alisema haijafika ofisini kwake, huku akisisitiza kuwa kama imeandikwa kwa Rais si lazima ifike kwake. “Sijaiona, ila kama wamemwandikia Rais barua sidhani kama itakuja kwangu. Itakwenda kwake moja kwa moja,” alisema Balozi Sefue. Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye hakutaka kuzungumzia hatua hiyo ya Chadema akisema, “Siwezi kusema chochote kwa kuwa barua yenyewe sijaiona pia ni barua ya Rais.” Kauli ya Bavicha Baraza la Vijana la Chadema (Bavicha), limemtaka Rais Kikwete kuunda tume huru yenye wataalamu wa sheria ili kuchunguza mauaji, utekaji, vurugu na unyanyasaji wa wananchi unaotokea kwenye mikutano ya siasa hasa inayokihusisha chama hicho.
Akizungumza na waandishi wa habari jana mjini Morogoro baada ya kikao cha baraza hilo taifa, Mwenyekiti wa Bavicha, John Heche alisema kwamba kama Rais Kikwete atashindwa kufanya hivyo, baraza lake kwa kutambua kuwa matukio mengi ya mauaji yamehusisha vijana, litahamasisha maandamano nchi nzima na kuishtaki Serikali yake. Habari hii imeandikwa na Fidelis Butahe na George Njogopa, Dar na Hamida Sharif, Morogoro. www.mwananchi.co.tz

Comments

Popular posts from this blog

MBINU ZA KUMFIKISHA MWANAMKE MWENYE MAKALIO MAKUBWA KILELENI KWA HARAKA

Kwa kawaida wanawake wanafikia kilele (mwisho wa utamu wa ngono) kati ya dakika ishirini na saa moja, yaani kwa kifupi inawachukua muda mrefu sana hali inayopelekea mpenzi mvivu kuchoka na ufanyaji wake utakuwa wa “ovyo” hali itakayo kufanya wewe kuishiwa na hamu ya kuendelea. Pamoja na kuchelewa huko ambako kunatokana na utofauti wetu kati ya mwanaume na mwanamke lakini nakumbuka hapo nyuma nilikutana na wanawake 2 waliokuwa ndani ya ndoa na wamezaa lakini hawajawahi kabisa kujua utamu wa tendo hilo alimaharufu kama “kufanya mapenzi”. Natambua kuwa ni ngumu au niseme si wanawake wote ambao wamejaaliwa kimaumbile kwamba wanafanikiwa kufika kileleni zaidi ya mara mbili kila wanapofanya mapenzi/ngono (kumbuka ni kati ya dakika 15 na saa moja hivyo Jibaba hapa awe na uwezo wa kujizuia kwa zaidi ya dk 45) na ikiwa jamaa ni “mzamiaji” basi unaweza ukaondoka na goli 3 ktk mzunguuko mmoja. Lakini kwa nini basi baadhi yao tu ndio wafike kileleni na wengine was...

Uganda Police issue fresh terror alert

  By Chris Kiwawulo, The Police have issued a fresh terror alert against a possible attack on Uganda by four terrorists from Kazakhstan. Police spokesperson Judith Nabakooba “We have received a security notification in form of an orange notice of four terrorists originating from Kazakhstan who are planning to travel to foreign countries in order to commit attacks and participate in hostile acts,” Police spokesperson Judith Nabakooba said in a statement on Monday. Nabakooba named the four active members of radical organizations as; Nassiruauly Kairat, Umurzakov Marat Eskendirovich, Kovtun Denis Valerevich and Mazhibayen Alimzhan Akhlazhanovich. By press time, a search on the international web has not yielded anything on the named persons.Last evening, police said that in collaboration with other security agencies vigilance has been stepped up to avert the terrorists’ evil plans. Police have in the past issu...

Poland’s GROM special services mastermind found dead

Brigadier General Slawomir Petelicki, responsible for the formation of the GROM special services unit in the 1990s, was found dead at his apartment, Saturday, with bullet wounds to the head. SÅ‚awomir Petelicki, 1946-2012. Photo: Archive/PAP/Radek Pietruszka Police spokesman Maciej Karczynski informed that Petelicki’s body was found by his wife in the garage of his Warsaw apartment on Saturday. He was 65. Primary investigations point to suicide as the cause of death. It is expected that prosecutors will decide on an investigation into Petelicki’s death on Monday. After examining the scene of the incident, “the body of General [Petelicki] has been taken to a forensic laboratory, although a post-mortem will probably take place on Monday,” prosecutor Katarzyna Calow-Jaszewska from the Warsaw District Prosecution told the PAP news agency. “He was a tough man, a brilliant soldier and commander,” Colonel Krzysztof Przepiorka, head of the ...