Taarifa
kwa vyombo vya habari.
Ligi
kuu ya Vodacom sasa mambo safi.
·
Sintofahamu kati ya
TFF na Klabu zafikia mwisho.
·
Vodacom yatoa fedha
na Vifaa kwa timu zinazoshiriki ligi kuu.
·
Yaahidi makubwa
zaidi.
Dar
es Salaam, 30 Septemba, 2012.
Kufuatia kukaa
katika kikao cha majadiliano kati ya Mdhamini mkuu wa ligi kuu Vodacom
Tanzania, kamati ya ligi, TFF na vilabu vinavyoshiriki ligi hiyo, Mashabiki
na wapenzi wa soka nchini wameondolewa hofu juu ya udhamini wa ligi
inayoendelea hivi sasa.
Mdhamini mkuu
wa ligi hiyo Vodacom Tanzania, imekubali kuendelea kuunga mkono ligi hiyo na
kuwaomba mashabiki wa soka kutegemea msimu mzuri wa ligi mwaka huu.
Kwa mujibu wa
Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania, Kelvin Twissa,
amesema kuwa mvutano ambao umekuwepo baina ya baadhi ya Vilabu vya soka na
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) pamoja na wadhamini sasa yamepatiwa
ufumbuzi.
“Kulikuwa na
sinto fahamu kati ya Klabu za ligi kuu TFF na sisi kama wadhamini, tulikaa
kikao siku ya ijumaa na wadau wote wa ligi na sasa mambo yote yamewekwa katika
msitari,” alisema Kelvin na kuongeza kuwa “ Tumedhamiria kuendelea kuiunga
mkono Ligi kuu ya Vodacom hatukuwa na matatizo yoyote katika kusaini mkataba na
kamati ya ligi ni ufafanuzi tu ndio ulihitajika ili kuwekana sawa,”
alisema Twissa.
Kuhusiana na
kutolewa kwa fedha za udhamini na uendeshaji wa ligi na udhamini wa kampuni
pinzania twissa alisema Vodacom haizuii klabu za ligi kudhaminiwa na kampuni nyingine
yoyote tofauti na zile zenye msingi wa kiushindani katika biashara na kampuni
hiyo.
“Kufuatia
kikao hicho na kuwa katika msitari mmoja tumekwisha toa fedha na vifaa kwa TFF
na vilabu ili ligi iweze kwenda kama ilivyo takiwa,Tukiwa kama wadau katika
kuunga mkono maendeleo ya soka nchini, tumeruhusu kampuni nyingine ambazo
hazina upinzani wa kibiashara na sisi ili kuondoa muingiliano wa kimaslahi,”
alisema.
“TFF
inadhamana ya kusimamia sheria na masharti kuhusu ligi. Hatuna matatizo yoyote
ya kiutendaji na TFF wala klabu yoyote” alihitimisha Twissa.
Ligi kuu ya
Vodacom ilianza rasmi tarehe 15 mwezi septemba, na tutashuhudia michezo
182 kwa kushirikisha timu 14 zinazoshiriki katika ligi hiyo, zikiwemo Yanga
Afrika, Kagera sugar, na Simba ambaye ndie bingwa mtetezi wa ligi kuu ya
Vodacom.
Kampuni ya Vodacom imekuwa mdhamini wa
ligi kuu kwa miaka mitano sasa, na imesaini mkataba mpya wa udhamini wa ligi
hiyo kwa miaka mitatu na shirikisho la mpira wa miguu TFF, mkataba utakao
shuhudia shirikisho hilo likipokea udhamini wa kila msimu kwa miaka mitatu
mfululizo.
Comments