Nadhani wengi wetu mnamtambua msanii,
Hafsa Kazinja ni mwanamuziki wa muziki aina ya Zouk kutoka nchini
Tanzania. Anafamika zaidi kwa kibao chake mashuhuri cha Presha presha.
Pia kibaochake ambacho nakizimia
cha Mashallah. Hasfa anatoka katika kikundi cha THT (yaani Tanzania
House of Talent) cha mjini Dar es Salaam.
Watanzania mliopo DMV mnaombwa
nyote kumuonga mkono dada yatu mpendwa msanii kutoka nyumbani Bibie
Hafsa Kazinja...(Masha-Allah), ambae anatarajiwa kufanya onyesho lake
siku ya Jumamosi Sept 22 maelezo yote ya anuwani na mpango mzima wa
onyesho hilo kabambe kutoka kwa msanii wetu, soma kwa kuzingatia Flayer
ilipo hapo chini.
Sikiliza kwa makini kibao chake cha Hafsa Kazinja Masha-Allah
Comments