Na Father Kidevu Blog na Bongostaz Blog, Morogoro
TIMU ya Yanga SC yenye maskani
yake Mtaa wa Jangwani jijini Dar es Salaam leo wameshindwa kupenya
katika Mashamba ya Miwa ya Mtibwa Suger FC ya Turiani mjini Morogoro
baada ya kuambulia kichapo cha aibu cha magoli 3-0 katika mchezo wa Ligi
Kuu ya Vodacom.
Kikosi kamili cha Yanga ambacho kimekubali kubebeshwa tani 3-0 za Sukari na Mtibwa Suger hii leo.
Wakati Yanga ikiambulia kichapo
hicho Mabingwa watetezi Simba SC ya Mtaa wa Msimbazi na mahasimu wakubwa
wa Yanga leo wamefanikiwa kuipindisha mitutu ya Askari wa Jeshi la
Kujenga Taifa kutoka Ruvu mkoani Pwani (JKT Ruvu) kwa magopli 2-0,
mchezo uliochezwa uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam.
Yanga iliyochini ya udhamini
mnono wa Kilimanjaro Lager na inayonolewa na Kocha Mbelgiji Tom
Saintfiet, ilishindwa kufurukuta kwa wakata miwa hao wa Manungu Turiani
wanao nolewa na Kocha Mzalendo na mchezaji wa zamani wa kikosi hicho na
kile cha Taifa Stars Meck Mexime.
Yanga ambayo imevuma sana katika
magazeti kuwa imefanya usajili wa uhakika kwa kuimarisha safu yake ya
Ulinzi ilianza kushushiwa Mvua ya magoli katika dakika ya 11 kipindi cha
kwanza.
Goli hilo la kwanza la wana Tam
Tam Mtibwa Sukari lilipachikwa kimiani na na beki wa kati, Dickson Daudi
akiunganisha kwa kichwa kona ya beki wa kushoto Malika Ndeule.
Niuzembe wa wazi wa mabeki wa
Yanga ndio uliosababisha goli hilo baada ya kushindwa kumuweka ulinzi
mchezaji mrefu kuliko wote, Daudi.
Comments