Edward aliyeingia kipindi cha pili kuchukua nafasi ya Ramadhani Chombo, alifunga bao hilo dakika 10 kabla ya mchezo kumalizika, kufuatia kazi nzuri iliyofanywa na Mrisho Ngasa.
Simba ilikuwa ya kwanza kupata bao kupitia kwa Felix Sunzi, aliyeunganisha wavuni kwa kichwa krosi maridhawa iliyochongwa na Nassoro Masoud Chollo aliyepanda mbele kusaidia mashambulizi.
Ruvu Shooting ilisawazisha bao hilo dakika ya 78 kwa bao lililofungwa na Seif Rashid baada ya kumpokonya mpira beki Juma Nyoso ndani ya eneo la hatari na kuukwamisha mpira wavuni.
Simba ilifanikiwa kupata penalti kipindi cha kwanza baada ya beki mmoja
wa Ruvu Shooting kuunawa mpira ndani ya eneo la hatari, lakini shuti la
Daniel Akuffour lilipanguliwa na kipa Benjamin Haule na kuwa kona,
ambayo haikuzaa matunda.Inatoka kwa mdau.
Comments