Rais wa Somalia aliyeondoka
madarakani Sheikh Sharif Sheikh Ahmed alikabidhi rasmi madaraka kwa
Hassan Sheikh Mohamud wakati wa sherehe za kutawazwa kwake katika Makao
makuu ya Chuo cha Polisi huko Mogadishu Jumapili (tarehe 16 Septemba).
Rais
wa Somalia Hassan Sheikh Mohamud akizungumza wakati wa sherehe za
kutawazwa kwake tarehe 16 Septemba jijini Mogadishu. [Mahmoud
Mohamed/Sabahi]
Sherehe hizo, ambazo
zilifanyika chini ya ulinzi mkali, zilihudhuriwa na watu wengi maarufu
wa kimataifa na kikanda, wakiwemo rais wa Djibouti Ismail Omar Guelleh,
Waziri Mkuu wa Ethiopia Haile Mariam Desalegn, Naibu waziri Mkuu wa
Uturuki Bakir Bozdag na Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika Jean
Ping.
Wawakilishi kutoka Uganda,
Sudan, Qatar, Sudan ya Kusini, Iran, Umoja wa Mataifa, Umoja wa Afrika,
Umoja wa Falme za Kiarabu na Asasi ya Ushirikiano wa Kiislamu pia
walihudhuria sherehe hiyo.
"Leo, Somalia na Jumuiya za
kimataifa zinashuhudia mtindo tofauti ambao haukuwahi kuonwa nchini
Somalia kwa miongo minne, ambao ni kukabidhi madaraka kutoka kwa rais
anayeondoka madarakani kwenda kwa rais aliyechaguliwa kidemokrasia,"
alisema mbunge, Mohamed Ahmed. "Hii ni mara ya pili katika historia ya
Somalia kutokea kwa ukabidhianaji wa madaraka "
Kwa mara ya kwanza ilitokea
miaka ya katikati ya 1960 wakati rais Aden Abdullahi Osman, Rais wa
kwanza wa Somalia baada ya uhuru, kukabidhi madaraka kwa rais
Abdirashid Ali Sharmarke.
Comments