Rais wa zamani wa Marekani Bill Clinton ametoa hotuba ya kina kumpigia debe Rais Barack Obama aweze kurejea ikulu kwa mhula wa pili katika uchaguzi wa rais mwezi Novemba.
Hotuba hiyo ya Clinton ilichukua dakika 49 muda ambao ndio mwingi zaidi kuliko wazungumzaji wengine katika mkutano mkuu wa Chama cha Democratic unaoendelea mjini Charlotte, jimbo la North Carolina.
Michelle Obama aliufungua mkutano huo mkuu wa
chama cha Democratic akimpigia debe mumewe
apewe muda zaidi
|
Huku akionekana kutofuata hotuba yake ya mandishi , Clinton alifafanua masuala muhimu ambayo hayajazungumziwa katika kongamano hilo. Aliusifu mpango wa kichocheo cha uchumi ambao Obama aliweka mnamo wa 2009, upanuzi wake wa msaada wa masomo ya vyuo na juhudi zake za kuboresha nishati mbadala.
Rekodi ya Obama yasifiwa
Alifafanua jinsi sheria ya Obama ya huduma za afya ilivyowanufaisha wamarekani wa kawaida, na akaonya kuwa pendkezo la Warepublican kupunguza matumizi ya huduma za afya kunaweza kuwaathiri watu masikini katika jamii. Alihoji kuwa warepublican huenda wakaendeleza matatizo ya kifedha ya nchi hiyo na kuwazuia watu zaidi dhidi ya kupiga kura.
Comments