Dar
es Salaam Young Africans wameendeleza mwanzo mbaya wa Ligi Kuu Tanzania
bara baada ya kukubali kichapo cha mabao 3-0 toka kwa wakata miwa
Mtibwa Sugar. Wakati huo Mnyama ameendelea kuunguruma uwanja wa Taifa
baada kuichapa JKT Ruvu 2-0 Kwa mabao ya Amri Kiemba na Haruna Moshi
Boban, pamoja na kucheza pungufu baada ya Emmanuel Okwi kupewa kadi
nyekundu kipindi cha kwanza.Inatoka kwa Mjengwa.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Ali Moh amed Shein,alipokuwa akifanya mahojiano na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa kupitia ZBC TV na kutoa wito kwa Watanzania hasa wa Zanzibar kushiriki kikamilifu katika zoezi la uandikishaji vitambulisho hivyo,ambapo zoezi hilo linatarajia kuwanza Oktoba 15 mwaka. Mazungumzo hayo yalifanyika Ikulu mjini Zanzibar leo,(kulia) Mtangazji wa ZBC TV Nasra Nassor. Picha na Ramadhan Othman,Ikulu

Comments