Viongozi
wa Mali wanajitayarisha na vita, kulikomboa eneo la kaskazini
linalodhibitiwa na makundi ya waasi wa Kiislamu: ni ujumbe kutoka Bamako
katika mkutano wa umoja wa mataifa,licha ya majirani zake kuwa na
shaka.
Tunahisi kuwa jumuiya ya kimataifa inawajibika kwa upande wetu, ikiwa ni
mshikamano na Mali, duru karibu na rais Dioncounda Traore ililiambia
shirika la habari la AFP.
Alikuwa akizungumza katika mkutano siku ya Jumatano mjini New York,
pembezoni mwa mkutano wa hadhara kuu ya umoja wa mataifa, ambao ulikuwa
unalenga kujadili kuhusu mzozo wa eneo la Sahel.
Maafisa wa Mali wanatambua kuwa majirani wa nchi hiyo Algeria inajaribu
kuleta hali ya maelewano na Mauritania na Niger ili kuzuwia uwekaji wa
majeshi ya kigeni nchini Mali, kimesema chanzo hicho.
Lakini Ufaransa itafanya kila linalowezekana kuhakikisha kuwa baraza la
usalama linakutana na azimio linaloidhinisha kuingilia kati
linapatikana, ameongeza afisa huyo.
Raia wanaunga mkono
Mjini Bamako , "watu hawaulizi tena lini vita vitaanza ?, lakini vipi
tunaweza kuweka pamoja masharti muhimu ya kuanzisha vita. Kwetu sisi,
uingiliaji kati hauko mbali sana, unatayarishwa, chanzo hicho kimeeleza.
Madou Diallo, profesa wa sheria za kimataifa katika chuo kikuu cha
mjini Bamako, jibu kutoka kwa jumuiya ya kimataifa limepunguka makali na
la kujizuwia zaidi.
Comments