Naibu Waziri wa Kazi na Ajira, Makongoro Mahanga (kulia) akimkabidhi
ngao ya jamii, nahodha wa Simba, Juma Kaseja baada ya timu hiyo kuichapa
Azam mabao 3-2 katika mechi iliyopigwa leo jioni kwenye Uwanja wa
Taifa, Dar es Salaam.SIMBA leo imefanikiwa kutwaa Ngao ya Jamii
baada ya kuicharaza Azam FC mabao 3-2 katika mechi iliyopigwa kwenye
Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.Mechi hiyo ni maalumu kwa ajili ya
ufunguzi wa michuano ya ligi kuu ya Tanzania Bara, inayotarajiwa kuanza
kutimua vumbi Jumamosi.Ushindi huo ulikuwa wa kulipiza kisasi kwa
Simba kufuatia kuchapwa mabao 3-1 na Azam katika mechi ya nusu fainali
ya Kombe la Kagame.Azam ilikuwa ya kwanza kupata mabao kupitia kwa
John Bocco na Kipre Tchetche kabla ya Daniel Akuffour kuifungia Simba
bao dakika chache kabla ya mapumziko na kuyafanya matokeo yawe 2-1.Simba
ilibadili mchezo kipindi cha pili na kufanikiwa kusawazisha kwa bao
lililofungwa na Emmanuel Okwi kabla ya Mwinyi Kazimoto kuongeza la tatu
na la ushindi.Inatoka kwa mdau.

Comments