Viongozi wa Mali wanajitayarisha na vita, kulikomboa eneo la kaskazini linalodhibitiwa na makundi ya waasi wa Kiislamu: ni ujumbe kutoka Bamako katika mkutano wa umoja wa mataifa,licha ya majirani zake kuwa na shaka. Tunahisi kuwa jumuiya ya kimataifa inawajibika kwa upande wetu, ikiwa ni mshikamano na Mali, duru karibu na rais Dioncounda Traore ililiambia shirika la habari la AFP. Alikuwa akizungumza katika mkutano siku ya Jumatano mjini New York, pembezoni mwa mkutano wa hadhara kuu ya umoja wa mataifa, ambao ulikuwa unalenga kujadili kuhusu mzozo wa eneo la Sahel. Maafisa wa Mali wanatambua kuwa majirani wa nchi hiyo Algeria inajaribu kuleta hali ya maelewano na Mauritania na Niger ili kuzuwia uwekaji wa majeshi ya kigeni nchini Mali, kimesema chanzo hicho. Lakini Ufaransa itafanya kila linalowezekana kuhakikisha kuwa baraza la usalama linakutana na azimio linaloidhinisha kuingilia kati linapatikana, ameongeza afisa huyo. Raia wanaunga mkono ...