Mkutano wa mgombea uteuzi wa chama cha Republic nchini Marekani
Donald John Trump katika jimbo la Chicago umeahirishwa kufuatia
maandamano.
Mkutano huo uliahirishwa kutokana na sababu za kiusalama baada ya
bilionea Trump kukutana na maafisa wa usalama katika eneo hilo.
Mamia ya waandamanaji hao wengi wao wenye asili ya Kiafrika na
Kilatini walighadhabishwa na matamshi ya Trump kuwahusu wahamiaji nchini
humo.
Wakosoaji wa Trump wameshutumu kwa kuchochea taharuki kwenye kampeini zake.
Mwaka 1968 ghasia zilikumba uteuzi wa chama cha Democrats katika
jimbo hilo hilo ulioandaliwa wakati ambapo kulikuwa na mgawanyiko nchini
humo kuhusu vita vya Vietnam.
Ghasia hizo zimejiri siku chache tu kabla ya kuandaliwa uteuzi wa
mchujo katika majimbo ya Florida, Ohio, Illinois na Missouri tarehe 15
mwezi huu, huku Trump akiwa kifua mbele katika uteuzi wa chama cha
Repiblican.
Comments