Kampuni inayochapisha majarida ya picha za utupu ya Playboy huenda
ikauzwa, ripoti nchini Marekani zinasema. Kampuni hiyo ya Playboy huenda
ikauzwa zaidi ya $500m (£354m), kwa mujibu wa duru zilizonukuliwa na
mashirika ya habari yakiwemo Wall Street Journal na Financial Times.
Taarifa hizo zimetokea wiki chache baada ya jarida hilo kutangaza lingeacha kuchapisha picha za utupu likisema ‘haziuzi’. Mauzo ya majarida hayo yameshuka sana na kufikia 800,000 mwaka jana kutoka 5.6m mwaka 1975.
Ripoti zinasema Investment bank Moelis & Co imeteuliwa kusimamia uuzaji wa biashara ya majarida hayo. Bw Hugh Hefner alianzisha Playboy mwaka 1953 huku mwigizaji mashuhuri Marilyn Monroe akiwa wa kwanza kupamba ukurasa wa jarida hilo ulioitwa "Playmate of the Month."
Jarida hilo lilipata umaarufu upesi sana.
Taarifa za kifedha za kampuni hiyo huwa hazipatikani kwa urahisi hasa baada ya Bw Hefner na kampuni ya uwekezaji ya Rizvi Traverse Management kufanya kampuni hiyo kuwa ya kibinafsi mwaka 2011. Lakini wakati wa mabadiliko hayo, Playboy ilikadiriwa kuwa na thamani ya $207m.
Kwa mujibu wa ripoti magazetini, ombi la kununua Playboy lilitolewa baada ya Bw Hefner kuanza kuuza jumba maarufu la Playboy Mansion mwezi Januari.
Comments