Rais John Pombe Magufuli amemteua Dkt. Ayub Rioba Chacha kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC).
Dkt. Ayub Rioba anachukua nafasi iliyoachwa na Clement Mshana ambaye amestaafu.
Kabla ya uteuzi huo Dkt. Ayub Rioba Chacha alikuwa Mkuu wa Chuo cha
Uandishi wa Habari na Mawasiliano kwa Umma (SJMC) cha Chuo Kikuu cha Dar
es Salaam.
Dkt. Ayub Rioba Chacha pia ni mwanasafu wa muda mrefu wa gazeti la Raia Mwema.
Mbali na uteuzi huo, Rais Magufuli amemteua Profesa Godius Kahyarara kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Hifadhi ya Jamii (NSSF).
Profesa Kahyarara anachukua nafasi iliyoachwa na Dkt. Ramadhan Dau aliyeteuliwa kuwa balozi mapema mwezi huu na Rais Magufuli.
Rais John Magufuli pia amemteua Dkt. Mussa Iddi Mgwatu kuwa
Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni hodhi ya rasilimali za reli Tanzania (RAHCO).
Dkt. Mgwatu anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Mhandisi Benhadard Tito, ambaye uteuzi wake ulienguliwa.
Comments