Kumekua na story nyingi za kwamba Drogba alikua na mpango wa ku-staff soka na kuwa assistant manager wa club ya Chelsea. Lakini leo hii Drogba amesema kwamba ataendelea kubaki kwenye club ya Montreal Impact.
Drogba ameiambia ESPN kwamba, “Kama ningeamua kurudi Chelsea ningerudi”. Drogba sasa hivi ana-recover kutokana na majeraha na kifundo cha mguu ameendelea kusema,“Msimu ni mrefu sana na pia kuna risk kubwa ya kucheza huu mchezo. Soo kwamba sitaki kucheza, naweza kucheza kwa sasa lakini tatizo ni kifundo changu cha mguu hadi nipone kamili”
Drogba hadi sasa amecheza mechi 14 na Montreal Impact na amefunga magoli 12.“Tangu nilipofika hapa focus yangu ipo kwenye team. Kila ninachowaza ni kucheza na kushinda. Nafanya kila kitu ninachoweza ili tufanye vizuri zaidi.”
Comments