REAL Madrid imebuni mpango wa kumnunua mshambuliaji wa Juventus, Alvaro Morata na kisha kumuuza bei mbaya kwa Arsenal ama Bayern Munich. Madrid ilimuuza Morata kwa Juve ‘Old Lady’ kwa pauni milioni 15.7 mwaka 2014, lakini ikaweka kipengele katika mkataba kwamba inaweza kumsajili tena straika huyo mwenye miaka 23 Julai 2016 au 2017 kwa ada ya pauni milioni 23.6. Mhispania huyo amekuwa kipusa tangu alipoondoka Bernabeu mwaka 2014, akifunga mabao 25 katika mechi 86 akiwa na jezi ya Juve, hali iliyoitamanisha Madrid kutaka kumrejesha nyumbani. Hata hivyo gazeti la AS la Hispania limeripoti kuwa mashabiki wa Madrid hawaonekani kupendezwa na kurejeshwa kwa straika huyo, hivyo klabu hiyo inaweza kumrejesha na mara moja kumuuza kwa bei mbaya. Inafahamika kuwa kuna klabu kadhaa zinazovutiwa na straika huyo hali inayompandisha thamani, zikiwamo Arsenal na Bayern Munich. Akizungumzia hali hiyo, Morata alisema anachotaka ni kuona wapi anaangukia. “Nataka suala hili la kununuliwa tena au la kumalizwa. Nina furaha Juve, lakini nataka kujua wapi nitakuwapo… Kurudi Madrid? Ni jambo lililopo na kweli linawezekana kwa sababu kuna mkataba, kuna nyaraka. Natazama mbele kwa hili kumalizika,” alisema.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Ali Moh amed Shein,alipokuwa akifanya mahojiano na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa kupitia ZBC TV na kutoa wito kwa Watanzania hasa wa Zanzibar kushiriki kikamilifu katika zoezi la uandikishaji vitambulisho hivyo,ambapo zoezi hilo linatarajia kuwanza Oktoba 15 mwaka. Mazungumzo hayo yalifanyika Ikulu mjini Zanzibar leo,(kulia) Mtangazji wa ZBC TV Nasra Nassor. Picha na Ramadhan Othman,Ikulu
Comments