Carson na Trump
Aliyekuwa
mgombea wa urais kupitia chama cha Republican Ben Carson amethibitisha
kwamba anamuunga mkono aliyekuwa mpinzani wake Donald Trump katika
kinyang'anyiro cha urais nchini Marekani.
Carson
alimuidhinisha katika mkutano wa pamoja na wanahabari mjini Florida huku
Trump akiwa anaongoza katika kura ya mchujo wa kumtafuta atakayewania
urais kupitia chama hicho kabla ya Jumanne kuu.
Bwana Carson ,aliye kifua mbele aling'atuka wiki iliopita baada ya kushindwa kuungwa mkono.
Ni mgombea wa pili kumuidhinisha bwana Trump baada ya Gavana wa jimbo la New Jersy Chris Christie.BBC
Comments