Hemedy
Msanii wa filamu na muimbaji wa R&B, Hemedy PHD amesema usumbufu anaoupata kwenye simu yake ni...
Msanii wa filamu na muimbaji wa R&B, Hemedy PHD amesema usumbufu
anaoupata kwenye simu yake ni mkubwa kiasi ambacho humfanya abadilishe
namba za simu kila mara.
Hemedy ameiambia Bongo5 kuwa anashindwa kutambua watu hao wanaipataje namba yake na kuanza kumsumbua.
Katika hatua nyingine Hemedy amesema kuwa wazazi wake pamoja na ndugu zao wamemshauri yeye na mpenzi wake kukaa kwanza pamoja ili kuendelea kusomana tabia kabla ya kufunga ndoa.
Hemedy ameiambia Bongo5 kuwa anashindwa kutambua watu hao wanaipataje namba yake na kuanza kumsumbua.
Nasumbuliwa sana mwanangu, dah mpaka noma, sijui hata nisemeje,” anasema Hemedy. “Meseji 600 kwa siku ni kitu cha kawaida. Sielewi tatizo ni nini, ukiona nalalamika hivi ujue naumia. Mpaka nikipigiwa huwa nafikiria kupokea simu. Mama yangu anapata usumbufu sana kwenye kusave namba yangu. Namba hii ni ya hamsini na moja tangu nianze sanaa 2008! Wanakuwa watu tofauti tofauti, lakini mademu ndo wanakuwa wengi.”
Katika hatua nyingine Hemedy amesema kuwa wazazi wake pamoja na ndugu zao wamemshauri yeye na mpenzi wake kukaa kwanza pamoja ili kuendelea kusomana tabia kabla ya kufunga ndoa.
Ndoa bado ipo, tena naweza sema ukaribu umeongezeka mara dufu. Lakini lakini kilichotokea ni suala la utayari kwa sababu kila mmoja anatakiwa awe tayari. Sasa watu wetu wa karibu pamoja na wazazi wametuambia ‘hebu jaribuni kufanya hivi, vuteni muda kidogo zaidi halafu tuone itakuwaje’ Pia hata mwanamke mwenyewe anahitaji kitu kidogo cha kutuhalalisha ila awe ni mke wangu.”.chanzo Bongo 5
Comments