Toto Zebingwa
BENDI mpya ya BMM inayoundwa na wanamuziki wa dansi imeanza kuja kwa kasi
na kupata heshima kubwa kwa wapenzi wa dansi, baada ya wiki iliyopita kuzinduliwa
kwa kishindo katika jiji la Dar es Salaam.
Bendi hiyo ilizinduliwa katika ukumbi wa Milenium Tower Kijitonyama,Dar es
Salaam ambapo inaundwa na mwanamuziki maarufu katika muziki huo Mule Mule
akisaidiwa na
mwanamuziki mwingine Toto Zebingwa ambao wote walipata kutamba vyema awali
katika bendi ya FM Academia.
Mkurugenzi Mkuu wa bendi hiyo, Thadey Jochim Mwacha anasema mapokezi ya
bendi hiyo katika hatua ya kwanza yameonesha hali kubwa ya mafanikio japo bado
wanajipanga zaidi.
"Niliweza kuona mageuzi wakati wa uzinduzi wa bendi hiyo, ambapo wakazi wa jiji
walijitokeza kwa wingi,"anasema Mwacha .
Wanamuziki wanaounda bendi hiyo wanasema
wao wanataka kuleta hali mpya katika mapinduzi ya muziki wa dansi nchini kurejesha
heshima yake.
“Tunahitaji mwezi mmoja tu kutoka sasa, mtakuwa mmeelewa kila kitu kuhusu wapi
tunapoelekea muziki wa dansi upo kwenye mazingira magumu, lakini kwa sasa
unaanza kurudi mahali pake, tutahakikisha tunafanya kazi itakayokidhi soko la sasa,”
anasema kiongozi wa bendi hiyo.
Kutokana na mazingira ya muziki huo kwa sasa kuonesha kuporomoka kwa haraka,
bendi hiyo inaonesha inaweza kuwa na mafanikio mengine
yatakayoonesha tija kwa wakati huu.
Bendi hiyo inaonekana imejipanga ambapo katika uongozi Toto Zebingwa ambaye
ni nyota katika bendi hiyo mpya ya BBM inayoongozwa Mule Mule, anasema
mambo mazuri yanakuja.
Toto Zebingwa amemzungumzia mkiongozi wake katika bendi hiyo, ambapo
anasema anamkubali Mule Mule anayeongoza kwa kuwa ni mtu wake wa karibu na
pia bendi inamipango ya kulitikisa jiji la Dar es Salaam na pia kurudisha heshima ya
muziki wa dansi.

Mule Mule
Mwanamuziki huyo anasema kuwa ndani ya muda mchache ujao, ukumbi wa New
Msasani Club walioanza kuutumia Jumapili iliyopita kwa kufanya Bonanza, ndio
moja kwa moja watakuwa wakiutumia.
Mwanamuziki huyo anasema bendi hiyo kabla ya uzinduzi rasmi, ilianza huku yeye
na Mule Mule wakishirikiana kwa mawazo kwa kiasi kikubwa na wamekuwa katika
urafiki wa kusaidiana katika changamoto nyingi kwa takribani miaka 17 iliyopita.
"Tulianaza kuwafuata matajiri wenye vyombo hivi vya muziki tukawa tunafanya
mazoezi kwa takribani miezi mitatu mpaka walipo tuona tupo katika wakati mzuri wa
kufanya makamuzi ndipo wakakubali tuanzishe bendi hii ya BBM,"anasema Totoo.
Anasema aliamua kumwachia nafasi ya uongozi wa juu mwanamuziki Mule Mule
kutokana na kumuona kama kaka yake waliopitia changamoto
nyingi katika maisha yao ya kimuziki.

Bendi hiyo imejipanga kufanya makamuzi katika siku ya Ijumaa, BBM Pub & Night Club iliyopo Mwenge na Jumamosi bendi hiyo itakuwa ikifanya onesho lake Meeda Sinza,Dar es Salaam ambapo kwa siku za Jumapili vinara wa bendi hiyo akiwemo
kiongozi wa bendi hiyo Mule Mule watakuwa wakifanya shoo katika Bonanza lao New Msasani Club.
Comments