Mtu mmoja ameuawa baada ya kubishana na rafiki yaje juu ya nani ni
mchezaji bora wa dunia kati ya Lionel Messi na Cristiano Ronaldo.
Raia mmoja wa Nigeria Michael Chukwuma, 21, alimchoma visu mwenzake Obina Durumchukwu katika mtaa mjini Mumbai, polisi wa India walisema.
Tukio hilo lilitokea kufuatia sherehe ya Jumamosi usiku.
“Walikuwa wakijadili kuhusu wachezaji soka. Mmoja ni shabiki wa Messi, mwingine alikuwa ni wa Ronaldo,” alisema polisi mchunguzi.
“Kuliibuka fujo wakati wa mazungumzo. Marehemu alirusha glasi usoni mwa mshtakiwa. Glasi ilipasuka na kusababisha majeraha kidogo usoni.”
“Baada ya hapo mshtakiwa alichukua glasi na kumshambulia nayo marehemu ambaye alifariki kutokana na kuvuja damu nyingi.”
Lionel Messi ameshinda tuzo ya mchezaji bora wa dunia mara tano, huku Cristiano Ronaldo akiondoka nayo mara tatu.

Comments