Conor McGregor alipigwa na Nate Diaz kwa kusalimu amri kwenye UFC 196.
McGregor alikubali kusalimu amri baada ya kukabwa koo katika raundi ya pili na Diaz mjini Las Vegas.
“Nimevunjika moyo. Nitaendelea kusikiliza nani mashabiki wangu wanataka nipigane naye kutetea mkanda wangu,” alisema McGregor.
Kwa upande wa wanawake Miesha Tate alimnyuka bingwa Holly Holm kwa kusalimu amri katika raundi ya tano.
Raia wa Ireland Conor McGregor atajiandaa kurudi Octagon kupambana na kati ya Jose Aldo au Frankie Edgar.
Comments