Maalim Seif yupo hotelini hapo kwa mapumziko baada ya kutolewa hospitali ya Hindu Mandal jana jioni alipokuwa amelazwa.
Maalim Seif amewahakikishia Watanzania kuwa afya yake inaendelea vizuri na kwamba anaendelea na shughuli zake na siku chache zijazo ana matumaini ya kurejea katika hali yake ya kawaida.
Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Sharif Hamad alilazwa katika hospitali ya Hindu Mandal jijini Dar es Salaam ikiwa ni siku tatu baada ya kutoka nchini India kimatibabu.
Comments