Roy Hodgson amemuita kwa mara ya kwanza kiungo wa Leicester City Danny Drinkwater, kwa ajili ya kikosi chake cha Euro 2016.
Drinkwater amekuwa kiungo muhimu Leicester inayopigania taji, na sasa
anajiandaa kuonyesha kuwa anastahili nafasi katika kikosi cha Uingereza
kitakachocheza mechi za kirafiki dhidi ya Ujerumani (Machi 26) na
Uholanzi Machi 29.
Mechi hizo mbili zitatumika kama mchujo wa mwisho kabla Hodgson
hajatangaza kikosi cha watu 23 kwa ajili ya Euro 2016 nchini Ufaransa
kwenye majira ya joto, wamo washambuliaji watano, akiwemo Danny Welbeck
na Daniel Sturridge.
Kikosi kamili;
Makipa: Butland, Forster, Hart
Mabeki: Bertrand, Cahill, Clyne, Jagielka, Rose, Smalling, Stones, Walker
Viungo: Alli, Barkley, Dier, Drinkwater, Henderson, Lallana, Milner, Sterling
Washambuliaji: Kane, Sturridge, Vardy, Walcott, Welbeck

Comments