Kwenye Nchi Ya Kusadikika Majipu Yanatumbuana Yenyewe..!
Ndugu zangu,
Nchi ya Kusadikika kamwe haiishiwi maajabu.
Wasadikika wamo kwenye mkanganyiko mkubwa ambao haujapata kutokea tangu kuundwa kwa taifa la Wasadikika.
Mwanafalsafa mashuhuri wa Nchi ya Kusadikika aitwaye Shaaban Robert alipata kubashiri mengi yanayotokea sasa kwenye Nchi Ya Kusadikika. Shaaban Robert miaka 80 iliyopita alipata kuelezea moja ya sifa za Wasadikika, kwamba hutafuta fimbo baada ya kuumwa na nyoka. Kwamba wanaweza kumwona nyoka lakini wasihangaike kutafuta fimbo ya kumpigia mpaka nyoka atawauma na kuwaachia sumu kali. Ndipo hapo Wasadikika hukumbuka fimbo.
Wasadikika wamempata kiongozi wao mkuu aliyeamua kupambana na nyoka wote wa Nchi Ya Kusadikika kabla hawajaleta madhara. Wasadikika wana hulka ya kuishi kwa mazoea, na hali hiyo mpya imewashangaza sana Wasadikika wengi, na hasa waposhuhudia majipu yakitumbuana yenyewe..!
Maggid,
Mwenyekiti wa Kitongoji Cha Kusadikika Kwenye Nchi Ya Kusadikika

Comments