Mkuu wa
Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda (kulia), akimvika kitambulisho Mkuu wa
Shule ya Sekondari ya Turiani, Beatrice Mhina Dar es Salaam jana
asubuhi, baada ya kuvizindua vitambulisho hivyo vitakavyotumiwa na
walimu kupanda daladala bure wakati wa kwenda kazini kufuatia mpango
aliouanzisha wiki iliyopita wa kuwasaidia walimu hao.
DC Makonda akimfika kitambulisho Mwalimu Gideon Mwenenyi.
DC Makonda akimvika kitambulisho, Mwalimu Ramadhani Korowelle.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda akizungumza na wananchi na walimu wakati wa uzinduzi wa vitambulisho hivyo.(P.T)
Ofisa Elimu wa Sekondari wa wilaya ya Kinondoni, Rogers Shemwelekwa (kulia), akizungumza katika uzinduzi huo.
Mwenyekiti wa Bodi ya Shule ya Sekondari ya Turiani, Alpherio Nchimbi (kushoto), akizungumza kwenye uzinduzi huo.
Walimu na viongozi wengine wakiwa kwenye hafla hiyo
Wananchi na walimu wakiwa kwenye uzinduzi huo.
Wananchi na walimu wakiwa kwenye uzinduzi huo.
Mwalimu Happyness Mailo (kushoto), akimshukuru DC Makonda kwa kuwawezesha mpango huo.
Mwakilishi wa wananchi, Ahmed Muhonga akimshukuru DC Makonda.
Mshairi, Msafiri Himba akitoa burudani kwenye uzinduzi huo.
Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Turiani, Beatrice Mhina akitoa neno la shukurani kwa DC Makonda.
Na Dotto Mwaibale
MKUU
wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda amezindua vitambulisho
vitakavyotumiwa na walimu kupanda daladala bure wakati wakitoka nyumbani
kwenda kazini.
Katika
hatua nyingine Makonda ameziomba sekta mbalimbali nchini kushiriki
katika kutoa mawazo yao ya maendejana ili taifa lizonge mbele badala ya
kuwa watizamaji.
Makonda
aliyasema hayo Dar es Salaam jana mbele ya wazazi na walimu wa Shule ya
Sekondari ya Turiani wakati akizindua vitambulisho hivyo
vitakavyotumiwa na walimu wa wilaya yake kupanda daladala bure kufuatia
mpango aliouanzisha wiki iliyopita wa kuwasaidia walimu hao.
“Nawaomba
watanzania na sekta mbalimbali kuwa na mawazo ya maendejana ambayo
yatawekwa mezani na kuyafanyia kazi jambo litakalo msaidia Rais wetu
Dk.John Magufuli katika kuliinua taifa kiuchumi badala ya kumuachia kila
kitu akifanye yeye” alisema Makonda.
Makonda
alitoa mwito kwa makondakta wa daladala kutoa ushirikiano kwa walimu
hao leo wakati watakapoanza kupanda magari yao huku wakijua walimu ndio
waliowafundisha na kufikia hatua hiyo ya kazi walizonazo.
Ofisa
Elimu wa Sekondari wa Wilaya hiyo, Rogers Shemwelekwa aliwaomba
wananchi hao na walimu kuendelea kuunga mkono jitihada za Makonda za
kuwaletea maendejana na kumuombea kwa mungu badala ya kumbeza kwani kazi
hizo anazozifanya ni kwa ajili ya wananchi.
(Imeandaliwa na mtandao wa www. habari za jamii.com
Comments